• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
      • Maji
      • Huduma ya Menejimenti ya Serikali za mitaa
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Menejimenti ya Serikali za mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Halmashauri zapewa Siku 14 Kuwalipa Wafanyakazi Bora

Imetumwa : May 1st, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos  Makalla ametoa siku 14 kwa  Halmashauri za Rungwe, Mbeya Jiji, Kyela na Busokelo kulipa madeni ya cheki  hewa za Wafanyakazi bora walizotunukiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika  mwaka 2016/2017.

Mhe Makalla ameyasema hayo leo kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Dunia (Mei Mosi) yaliyofanyika kimkoa  katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine yakiwa  na Kauli Mbiu ya “ Unganishwaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii ulenge kuleta tija kwa wafanyakazi”.

“ Natoa  siku 14 kwa Halmashauri zote zilizotajwa kurejesha fedha hizo kwa wafanyakazi bora walitunukiwa kwa sababu halmashauri  mnapenda kutengeneza madeni yasiokuwa  ya lazima. Na siku ya leo sitatoa cheki bila kuwa na fedha taslimu”. Amesema

Mhe Makalla amesema kuwa inasikitisha sana kwa Halmashauri  kubwa kama Mbeya Jiji kutokuwa  na uwezo wa kuwalipa fedha taslimu wafanyakazi wake bora na  kutoa ahadi zisizokuwa  na utekelezaji kwa muda mrefu sasa.

Akisoma risala Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha Huduma na Ushauri (TUICO) Kanda za Nyanda za Juu Kusini Merboth Kapinga ametoa malalamiko kwa halmashauri  hizo kutoa cheki  hewa za wafanyakazi  bora katika maadhimisho hayo mwaka 2016/2017.

Kapinga amesema kumekuwepo na utamaduni katika baadhi ya waajiri kuteua wafanyakazi bora katika vitendo mbali mbali na siku ya maadhimisho hawatoi fedha bali maneno matupu  na kusababisha kuwafunja  moyo wa utendaji na hasa kwa watumishi  wanaokaribia kustaafu.

Kapinga amemuomba Mkuu wa Mkoa kukemea jambo  hilo lisijirudie tena kwani kuna baadhi ya Halmashauri mpaka leo hawajawalipa  wafanyakazi mpaka wamestaafu utumishi wao.

Aidha Mhe.  Makalla amewaonya  Watumishi wa Serikali kuacha matumizi mabaya  ya mitandao ya kijamii  na kuacha  kufanya kazi kwa mazoea ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano  ili kuweza  kutatua matatizo  ya wananchi sehemu za kazi kwa wakati.

Amesema kuwa ipo kasumba ya baadhi ya wafanyakazi wanapoingia maofisini  jambo kubwa ni kufungua mitandao ya kijamii bila kujali wananchi wanaosubiria huduma jambo ambalo serikali haikubaliani nalo na kuwataka waajiri  kufuatilia  kwa ukaribu  ili kurejesha nidhamu ya utendaji kazi .

Mhe Makalla amekiri Serikali kutambua changamoto za Wafanyakazi hususani kiwango cha kima cha chini cha mshahara, makato  makubwa  ya kodi na tozo mbali mbali, upandishwaji wa vyeo na madeni  ya watumishi  ambapo tayari Serikali imeanza kushulikia changamoto hizo.

Amesema kuwa wakati Serikali ikiangalia na namna ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi waajiri watengeneze watengeneze  mazingira mazuri na wezezeshi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanajiunga  katika mifuko  ya kijamii wanayotaka  na si kuwachagulia jambo ambalo linawanyima uhuru na haki sehemu za kazi.

Mwenyekiti wa TUICO Mkoa wa Mbeya Bibi Winfrida Mnandi amewahimiza wafanyakazi kazi kwa nidhamu katika maeneo yao ya kazi ili kuhudumia  wananchi kwa wakati na bila upendeleo na kuwaasa  waajiri kuwa karibu na watumishi wao ili kufuatilia utendaji kazi wao.



Matangazo

  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato chaKwanza 2020 Mkoa wa Mbeya. December 06, 2019
  • Matokeo ya Darasa la Saba 2019 October 17, 2019
  • Fomu za Kujiunga na Kidato cha Tano 2019 June 10, 2019
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2019 Mkoa wa Mbeya. December 17, 2018
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • Mkuu wa Mkoa Awataka Watumishi Kuacha Urasimu

    November 29, 2019
  • Usuluhishi wa Mgogoro wa Ardhi kati ya Wananchi wa Kijiji cha Nanyara na Kiwanda cha Songwe

    November 02, 2019
  • Miradi ya Sh Bilioni 26 Kutembelewa na Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019

    September 03, 2019
  • Waziri Mkuu Mstaafu Mh Pinda Afunga Maonesho ya Nanenane Mbeya

    August 08, 2019
  • Tazama Zaidi

Video

Viongozi watakiwa kuwa wasafi
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Bajeti ya Mkoa wa Mbeya 2018/2019
  • Mpango wa Bajeti 2018/2019
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Fomu ya Ruhusa
  • OPRAS Fomu
  • Maoni na Malalamiko
  • Mwongozo Uwekezaji Mkoa wa Mbeya
  • Mafanikio ya TASAF

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Ajira

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Uzunguni Road

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 022 253034

    Simu ya Mkononi: 255 784838650

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2019 Mbeya Region . All rights reserved.