• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
      • Maji
      • Huduma ya Menejimenti ya Serikali za mitaa
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Menejimenti ya Serikali za mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Halmashauri zatakiwa Kutenga Fedha za Afua za VVU na UKIMWI

Imetumwa : December 1st, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila ameziagiza halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya kutenga fedha kutoka vyanzo vya ndani ili kuendelea kutekeleza afua VVU na UKIMWI hasa kwa kinga na tiba ili kufikia malengo ya Mkoa ya kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.

Mhe Chalamila ametoa maagizo hayo leo Disemba 1, 2020 kwenye maadhimisho ya kilele cha Siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika viwanja vya Barafu Kata ya Rujewa Wilaya ya Mbarali na kusema kuwa kunahitajika rasilimali za kutosha hasa kipindi kwa kuwa rasilimali kutoka kwa wadau zimepungua kwa kiasi kikubwa.

Amesema kuwa Ili kuongeza kasi ya kuzuia maambukizi mapya ya VV na hatimaye kutokomeza kabisa maambukizi hayo, Mkoa kwa kushirikiana na wadau wengine, umeamua kutekeleza mikakati ya kuzuia maambukizi mapya ya VVU kwa njia mbalimbali kama: kutoa elimu ya mabadiliko ya tabia, ushauri nasaha na upimaji wa VVU ,  upimaji binafsi wa VVU, tohara kwa wanaume nk.

Mhe Chalamila amesema kuwa kutokana na takwimu za utafiti wa viashiria vya UKIMWI ya mwaka 2016/17 inaonyesha maambukizi ya VVU ni makubwa kwa kundi la vijana na hasa  mabinti wa umri wa kati  ya miaka 15-24.

“Kwa kweli tukikaa kimya hali Mbeya ukiangalia hata matukio ya kubaka yameshamili sana jambo ambalo ni kichochoe kwa hali ya kupanda kwa maambukizi na kufikia asilimia 9.3 kimkoa na kufika nafasi ya tatu kitaifa

Akisoma taarifa ya Mkoa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt Salum Manyata amesema   kuwa Mkoa wa Mbeya umeshika nafasi ya tatu kitaifa kwa kuwa na asilimia 9.3 ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi huku waathirika wakubwa ni wasichana wenye wa chini ya miaka 24 kwa asilimia 70.

Dkt Manyata amesema  kuwa sababu kubwa ya kundi kuathika kwa kiwango hicho ni kutokaa na mihemko ya kushiriki tendo la ndoa wakiwa na umri mdogo hususan kwa watu waliowazidi umri.
"Licha ya wasichana pia asilimia 30 ya vijana ni wahanga hivyo kuna kila sababu ya kuwa na mpango mkakati wa pamoja ili kunusuru kundi hilo kwani ni nguvu kazi kwa taifa katika kuelekea uchumi wa viwanda "alisema

Aidha amesema kuwa takwimu zinaonyesha vijana walio katika kundi hilo 200 kwa siku wanambukizwa ukimwi huku kwa mwezi ni 6,000 hivyo ni jukumu la wadau mlioshiriki maadhimisho hayo kutafuta mwarobaini wa pamoja ili kuiweka Tanzania ikiwa Salama.

Mratibu wa tume ya kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Mkoa Emmanuel Petro, alisema kwa kipindi cha Oktoba 2019 mpaka Septemba mwaka huu jumla ya wakazi 217,762 walipima afya ambapo 11,185 walipatikana na maambukizi mapya ya Virusi vya ukimwi.Aidha alisema kwa kipindi hicho wajawazito 81,525 walipimwa ambapo kati ya hao 2,063 walikutwa na maambukizi na kuanza kupatiwa tiba na afya zao zinaendelea vizuri.

Matangazo

  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza 2021 Mkoa wa Mbeya. December 18, 2020
  • Matokeo ya Kidato cha Sita 2020 August 21, 2020
  • Matokeo ya Darasa la Saba 2020 November 21, 2020
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • Mkoa wa Mbeya Wajiwekea Malengo ya Upandaji miti

    January 13, 2021
  • Mbeya Yaja na Mkakati Mpya wa kupunguza Upungufu wa Vyumba Vya Madarasa

    December 09, 2020
  • Mbeya Waadhimisha Siku ya Uhuru kwa Kupanda Miti

    December 09, 2020
  • RC Aagiza Kuchunguza Upotevu wa 800M za Walimu

    December 04, 2020
  • Tazama Zaidi

Video

Viongozi watakiwa kuwa wasafi
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Wasifu wa Mkoa wa Mbeya 2015
  • Mpango Mkakati wa Mkoa 2018-2023
  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Mpango Mkakati wa Kuendeleza Sekta za Kilimo 2020 - 2025
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Ajira

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Uzunguni Road

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025 2503034

    Simu ya Mkononi: 255 784838650

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2019 Mbeya Region . All rights reserved.