• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
      • Maji
      • Huduma ya Menejimenti ya Serikali za mitaa
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Menejimenti ya Serikali za mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Sita Wakamatwa kwa Kughushi Saini

Imetumwa : November 27th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ameamuru watu sita kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kughushi saini za watu waliofariki dunia kisha Serikali kuwalipa fidia ya Sh108 milioni katika eneo lenye mradi wa soko.

Chalamila amesema hivyo leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Iyunga jijini hapa ambako kuliibuka mgogoro wa eneo la soko huku watuhumiwa hao wakidai ni mali yao.

"Hawa wazee walifika ofisini kwangu na kuandika barua ofisi ya Rais na Waziri Mkuu waidai fidia ya Sh 108 milioni huku halmashauri ikiwa imewalipa fidia ya Sh 17 milioni ambazo ni halali na walipisha eneo hilo "amesema.

Chalamila anasema baada ya kuwasikiliza malalamiko yao amelazimika kuchunguza kwa kina na kubaini kuwa watuhumiwa hao ni matapeli tayari walilipwa fidia na kwamba kiwanja hicho chenye mradi wa soko ni eneo la urithi wa Wazazi wao ambao walipewa bure na kiongozi wa kimila na hivyo kufanya utapeli kwa serikali.

Mmoja wa watuhumiwa hao, Philimon Chapanga amekiri mbele ya umati wa watu kuwa walilipwa Sh 17 milioni na kwamba hawajaridhishwa na kiwango hicho cha fedha kwa kuwa eneo hilo la mradi wa soko lilikuwa kwa ajili ya kilabu cha wazee kujiliwaza jioni.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Amude Ng'wanidako amesema watuhumiwa hao walilipwa Sh.17 milioni ikiwa ni fidia ya mradi wa soko ambalo kwa sasa ni mali ya serikali .

Amesema kimsingi madai hayo si ya kweli ni suala la kuihujumu Serikali kwa madai ya fidia Sh 108 milioni.

"Mgogoro huu ni wa miaka mingi baada ya kufualia nyaraka na kamati zilizoundwa kufuatilia nimebaini wahusika hawaidai halmashauri na kwamba eneo la soko ni mali ya Serikali,” amesema.

Akizungumza katika mkutano huo, Nelson Mayena mzee wa mila aliyetoa eneo hilo (chifu Mayena) amesema lilitolewa bure kwa watuhumiwa na walijenga klabu cha wazee kwa ajili ya maongezi ya jioni na kwamba awali walikubaliana na Serikali kulipwa fidia na kupisha mradi wa soko.

Matangazo

  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza 2021 Mkoa wa Mbeya. December 18, 2020
  • Matokeo ya Kidato cha Sita 2020 August 21, 2020
  • Matokeo ya Darasa la Saba 2020 November 21, 2020
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • Mkoa wa Mbeya Wajiwekea Malengo ya Upandaji miti

    January 13, 2021
  • Mbeya Yaja na Mkakati Mpya wa kupunguza Upungufu wa Vyumba Vya Madarasa

    December 09, 2020
  • Mbeya Waadhimisha Siku ya Uhuru kwa Kupanda Miti

    December 09, 2020
  • RC Aagiza Kuchunguza Upotevu wa 800M za Walimu

    December 04, 2020
  • Tazama Zaidi

Video

Viongozi watakiwa kuwa wasafi
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Wasifu wa Mkoa wa Mbeya 2015
  • Mpango Mkakati wa Mkoa 2018-2023
  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Mpango Mkakati wa Kuendeleza Sekta za Kilimo 2020 - 2025
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Ajira

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Uzunguni Road

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025 2503034

    Simu ya Mkononi: 255 784838650

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2019 Mbeya Region . All rights reserved.