• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

269 Milioni Zatolewa Kwa Wanawake,Vijana na Walemavu

Imetumwa : March 12th, 2021

Jiji la Mbeya limetoa kiasi cha Shilingi 269,501,500.00 kwa makundi matatu ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021

Fedha hizo zimetolewa kwa vikundi 32 vilivyokidhi vigezo vya kupatiwa mkopo katika robo hii ya pili, ambapo kati ya hivyo vikundi vya wananwake 22 vimepatiwa jumla ya fedha kiasi cha Shilingi 169,000,000.00, vijana  vikundi 7 vimepatiwa jumla ya Shilingi 75,000,000.00 na watu wenye ulemavu vikundi 3 na wenyewe wamepatiwa kiasi cha Shilingi 25,000,000.00

Akisoma taarifa ya Mikopo hiyo Afisa Maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya ndugu Vincent Msolla aliwaeleza wananchi waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya kuwa lengo kuu la kutoa mikopo hiyo ni kuwaimarisha wananchi kiuchumi na kuongeza kipato kwa wananchi wasio na ajira

Nae Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Bwana Amede Ng’wanidako alieleza kuwa Mikopo hiyo iliyotolewa na ofisi yake ni moja ya utekelezaji wa sera za nchi kwa kutoa sehemu ya asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwaajili ya kuwakopesha makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa uwiano wa asilimia 4 kwa wanawake, asilimia 4 kwa vijana na asilimia 2 kwa watu wenye ulemavu

Akikabidhi Mikopo hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Albert Chalamila aliwataka wanufaika wa Mikopo hiyo kurejesha kwa wakati mikopo yao ili iweze kuwanufaisha wananchi wengine” Hela hizi sio hisani ni hela za serikali hivyo ni vyema ukipewa mkopo huu ukarejesha kwa wakati ili na wengine wapate kunufaika”  alieleza RC Chalamila

Aidha RC Chalamila amewataka wanufaika hao kutumia Fedha hizo kwa shughuli za kibiashara na si vinginevyo, hizi sio fedha za mchango wa harusi au msiba aliongeza RC Chalamila

Akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Mheshimiwa Dormohamed Issa Rahmat alimhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuwa atatembelea vikundi vyote vilivyopatiwa Mkopo ili kuweza kuona maendeleo ya vikundi hivyo

Hii ni awamu ya pili ya utoaji wa Mikopo kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021 huku awamu ya kwanza Halmashauri ya Jiji la Mbeya ikitoa Mikopo yenye thamani ya Shilingi 260,000,000.00 kwa vikundi 27 ambavyo vikundi vya wanawake vilikuwa vikundi 15, vijana 6 na vikundi vya watu wenye ulemavu 6

Mpaka sasa katika kipindi cha robo ya kwanza na ya pili, tayari Halmashauri imeshatoa kiasi cha Shilingi 529,501,500.00

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA IMES

    April 29, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YARIDHISHWA NA MAJIBU YA WADAU KUHUSU MAPENDEKEZO UGAWAJI WA JIMBO LA MBEYA MJINI.

    April 25, 2025
  • DKT. HOMERA AAGIZA MRADI KUKAMILIKA HARAKA IWEZEKANAVYO ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA

    April 14, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa