• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

7 Irrigation Scheme were penalized by National Task Force for Evaluate Ruaha River Ecology

Imetumwa : April 27th, 2017

Kikosi Kazi cha Kitaifa cha kutathmini  Ikolojia ya Mto Ruaha kimeadhibu kwa kutoza faini ya jumla ya shillingi 180,290,000 skimu 7 za umwagilija za  Iyala, Ukwavila- Nguvukazi, Madibira, Mwendamtitu, Mbarali Estate, Kapunga na Kapunga Smallholders zilizopo Wilaya ya Mbarali kwa kutozingatia  sheria za Mazingira, Umwagiliaji  na kutumia maji bila kupata kibali cha matumizi kutoka Mamlaka husika.

Akiongea kwa niaba ya Wajumbe wa Kikosi Kazi hicho Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi amesema kuwa skimu hizo zimetozwa faini baada ya kugundua baadhi ya skimu zinatumia mifereji ya matoleo ya maji na kuchepusha maji hayo kwenda kwenye mashamba bila utaratibu na kibali.

Bw. Muyungi amesema kuwa Skimu za Kapunga, Highland Estate na Madibira zimetozwa faini kwa kutozingatia sheria ya Mazingira, Maji na kutosafisha mifereji ya kuingiza na kutolea maji na kufanya maji mengi kutotiririka kuelea kwenye Mto Mbarali na Ndembela  na kusababisha mito hiyo kupungua maji.

Faini hizo zimetozwa kwa kufuata sheria za Mazingira, Maji pamoja na Umwagiliaji kwa mchanganuo  kwa kila skimu ambapo Iyala wametozwa shilingi 2,200,000, Kapunga Farm shilingi 33,100,000, Mbarali Estate shilingi 33,000,000 Kapunga Small Holders shilingi 3,000,000 Madibira shilingi 33,000,000 Mwendamtitu shilingi 37,995,000 na Ukwavila- Nguvu Kazi shilingi 37,995,000.

Aidha Mwenyekiti wa Kikosi Kazi hicho ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bibi Mariam Mtunguja amesema kuwa faini hizo zinaenda sawa na maagizo waliyopewa skimu zote ya kufanya marekebisho ya miundombinu ya shamba ikiwa pamoja na kusafisha miundombinu hiyo na kuomba kibali cha matumizi ya maji kwa kuzingatia taratibu na sheria.

Bibi Mtunguja amesema Kikosi kazi kimetoa muda wa mwezi mmoja na nusu kwa wakulima wanatumia maji bila kibali kuvuna mazao yao yaliopo shambani na baada ya hapo mashamba hayo yatafungiwa mpaka pale wakulima hao watakapo pata kibali cha matumizi ya maji.

Naye Mwenyekiti wa muda wa Wakulima wa Kijiji cha Iyala Bwana Lenard Mwashikamile amekiri kuwa wakulima wa Kijiji hicho wanatumia maji kutoka kwenye mifereji ya matoleo ya mwekezaji bila kibali na kuomba wapewe muda wa kumalizia msimu huu wa mavuno.

Bwana Mwashikamile amesema kuwa kutokana na uhaba wa mvua msimu huu wamekuwa wakichepusha maji kutoka kwa mwekezaji kwa ajili ya matumizi ya umwagiliajia mashamba yao ya mpunga  pamoja na mifugo na wakijua kuwa ni kinyume cha taratibu na kuahidi kufunga miferji hiyo baada ya msimu huu wa kilimo.

Naye Afisa Uhusiano wa Mashamba ya Kapunga Bwana James Maliki ameshukuru Kikosi Kazi kwa kujionea maendeleo ya shamba la Kapunga na kuliweka katika hali nzuri na kukiri kuwepo kwa wakulima jirani na mashamba hayo kuiba na kutumia maji bila Kibali na kuahidi kuanza kushughulikia suala hili kwa kuweka ulinzi wa kutosha na kuweka matuta kwenye mifereji ya matoleo.

Kikosi Kazi cha kutathmini Ikolojia ya mto Ruaha kiliundwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu kwa lengo la kupata maoni na changamoto za wadau kuhusu kupungua kwa maji katika Hifadhi ya Ruaha na mabwawa ya Kidatu na Mtera.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA IMES

    April 29, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YARIDHISHWA NA MAJIBU YA WADAU KUHUSU MAPENDEKEZO UGAWAJI WA JIMBO LA MBEYA MJINI.

    April 25, 2025
  • DKT. HOMERA AAGIZA MRADI KUKAMILIKA HARAKA IWEZEKANAVYO ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA

    April 14, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa