• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Afisa Madini Atakiwa Kuweka Bei za Madini kwenye Migodi

Imetumwa : April 13th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila amemtaka Afisa Madini Mkazi Wilaya ya Chunya kubandika bei ya soko la madini kila inapobadilika kwenye migodi yote ya wachimbaji wadogo ili waweze kuepuka kudhulumiwa madalali wa madini.

Mhe Chalamila ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea na wachimbaji wadogo wa Isoko wilayani Chunya na kusema kuwa bei ambayo wachimbaji wadogo wanauza kwa madalali (brokers)  imekuwa ni ndogo kuliko ya sokoni

“tarehe 2/05/2019 tulifungua soko la madini pale Chunya mjini, tulipofungua tulitegemea watu wakauzie  madini pale lakini bado kumekuwa na tabia kuja kuwadalalia hapa wachimbaji wadogo wadogo, bei iliyopo sokoni na wewe unayeuza hapa inakuwa ni Mbingu na Ardh”. Mhe Chalamila

Amesema kuwa  wanachofanya madalali hao ni unyanyasaji na unyonyaji na ni utapeli ambao hautawezwa kuendelezwa katika Mkoa wa Mbeya na kuwaomba madalaliambao wanakuja kununua madini kwa wachimbaji wadogo na kuwauzia wanunuzi kutowanyanyasa na kuwaonea wachimbaji wadogo. , 

Naye Mchimbaji Mdogo Bw. Ahobokile Mwasyeba mbali na kupongeza juhudi zinazofanywa na Mkoa na Halmashauri ya wilaya ya Chunya kufungua soko hilo alieleza manufaa ya soko hilo kuwa ni pamoja upatikanaji wa wanunuzi wa uhakika wa madini hayo na bei elekezi inayotolewa na Serikali

Ahombwile ameeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa soko la madini bei ya gramu moja ya dhahabu haijawahi kupungua chini ya 90,000 tofauti na awali ambapo walikuwa wanauza kwa bei ya hasara.

Naye Akizungumza Mmiliki wa Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Mdimi Investment C. Limited, Mdimi Msigwa leo, Serikali imeweka mazingira rafiki na salama kwa wafanyabiashara na wachimbaji wa madini kwa kuwaanzishia masoko ya madini, hivyo hakuna haja ya kutorosha madini.

Msigwa alieleza kuwa, kabla ya kuanzishwa kwa soko hilo alikuwa na uwezo wa kuajiri wafanyakazi wachache kutokana na dhahabu yake kutokuwa na soko la uhakika na kuongeza kuwa baada ya uanzishwaji wa soko aliweza kuongeza ajira kutokana na biashara ya madini ya dhahabu kuwa ya uhakika.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA IMES

    April 29, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YARIDHISHWA NA MAJIBU YA WADAU KUHUSU MAPENDEKEZO UGAWAJI WA JIMBO LA MBEYA MJINI.

    April 25, 2025
  • DKT. HOMERA AAGIZA MRADI KUKAMILIKA HARAKA IWEZEKANAVYO ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA

    April 14, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa