• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Viongozi wa Wilaya na Halmashauri Kufanyiwa Tathmini

Imetumwa : December 7th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla awataka viongozi wakuteuliwa kufanyiwa tathmini kujua uhamasishaji waliofanya kuhusu ujenzi wa Vituo vya Afya kila Kata na Zahanati kila Kijiji Ilani, Viwanda pamoja na masuala ya Elimu katika Mkoa kama ya Chama cha Mapinduzi.

Akiongea katika Ufunguzi wa Kikao cha Afya Mkoa Mhe. Makalla amesema utekelezaji wa Afya ya Msingi unasuasua ambapo hadi kufikia Septemba 2017, Mkoa una Vituo vya tiba 310 vikijumuisha Hospitali 15, Vituo vya Afya 25 na Zahanati 270 ambapo Zahanati 37 zipo katika Jiji la Mbeya. 

Mhe. Makalla amesema kuwa Mkoa una jumla ya vijiji 553 na idadi ya Zahanati ni 233 sawa na asilimia 43.7 ya idadi ya vijiji.  Aidha, mkoa una Kata 178 na vituo vya afya vilivyopo ni 25 sawa na asilimia 14 ya idadi ya Kata

Mhe. Makalla amesema kuwa wa mujibu wa Sera ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) ya mwaka 2007 inaelekeza kila kijiji kiwe na zahanati na kila Kata iwe na kituo cha afya. Afya ya Msingi ikiboreshwa inasaidia kupunguza muda mwingi ambao mwananchi anatumia kutafuta huduma za afya kwa sababu vijiji vingi havina Zahanati.

“Viongozi wa Wilaya na Halmashauri mnatakiwa Kuhamasisha uboreshaji wa afya ya Msingi kwa wananchi kwa sababu ni mojawapo ya vipaumbele vya Mkoa. Wananchi hawajahamasishwa vya kutosha kuhusu ujenzi wa vituo vya afya na Zahanati na Serikali ipo tayari kuweka harambee katika kila zahanati zinazohitaji kupauliwa”

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk. Yahya Msuya amesema kuwa moja ya malengo ya Kikao hiki ni kuweka mkazo wa ujenzi wa Vituo vya afya kila Kata na na Zahanati kila Kijiji ili kuendana sawa na vipaumbele vya Mkoa katika kuboresha Afya ya Msingi.

Dkt. Yahya Msuya amesema kuwa Mkoa lengo la Mkoa ni kujenga zahanati 4 na vituo vya afya 2 katika kila Halmashauri kwa mwaka ili kuondoa upungufu huo.  Hadi kufikia Oktoba 2017 jumla ya Zahanati 7 kati ya 103 zimekamilika (Mbeya Jiji 1, Chunya 3, Mbeya DC 1, na Mbarali 2) na zahanati 96 zipo katika hatua mbalimbali ya ujenzi. 

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA IMES

    April 29, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YARIDHISHWA NA MAJIBU YA WADAU KUHUSU MAPENDEKEZO UGAWAJI WA JIMBO LA MBEYA MJINI.

    April 25, 2025
  • DKT. HOMERA AAGIZA MRADI KUKAMILIKA HARAKA IWEZEKANAVYO ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA

    April 14, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa