Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera ameahidi kuendelea kutekeleza yale ambayo mtangulizi wake aliyaanza na kubuni mambo mapya kwa ajili ya kuendeleza Mkoa wa Mbeya
Mhe Homera ametoa kauli hiyo leo Mei 21, katika halfa fupi ya makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika baina yake na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Albert Chalamila katika Ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya
Homera ameeleza kuendelea kushirikiana na taasisi zote zilizopo ndani ya Mkoa wa Mbeya na kutegemea kupata ushirikiano kama aliopewa mtangulizi wake
Ameongezea kuwa anatambua Mkoa wa Mbeya una changamoto zake na moja ya changamoto ni ukosefu wa miundombinu lakini ili kufanikisha ameahidi kukutana na wasimamizi kwa lengo la kushauriana na kubuni njia ya kuondokana na matatizo hayo
Aidha, Homera amesema kuwa atahakikisha anakutana na makundi mbalimbali yakiwemo bajaji, daladala, wafanyabiashara na wamachinga kwa lengo la kuhakikisha kila mtu anakuwa na furaha sehemu anayofanyia kazi yake.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Albert Chalamila amewashukuru watendaji wote wa Taasisi za Seikali na Binafsi kwa ushirikiano waliompa wakati wa uongozi wake na kuwata kuendelea kutoa ushirikiano huo kwa Mkuu wa Mkoa wa sasa
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa