• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kongamano la Uwekezaji

Imetumwa : September 27th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla amesema Mbeya umeendelea kuunga mkono jitihada hizo za Serikali kwa vitendo kwa kujenga miundombinu muhimu kwa ajili ya uwekezaji kama vile barabara, kujenga miundombinu ya umwagiliaji, umeme, kuimarisha hali ya ulinzi na usalama na mengine.

Mhe. Makalla ameyasema hayo katika Kongamano la Uwekezaji la Mkoa wa Mbeya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati Mkoa uliyojiwekea kama Mkoa kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa Mkoa wetu kwa kuwashirikisha wadau wote wa sekta ya umma na binafsi.

“Tunatambua jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii ili kufikia uchumi wa kati. Uwekezaji huu unafanywa kwa namna mbalimbali ikiwemo ya ubia kati ya sekta ya umma na binafsi” Mhe Makalla

Uchumi wa Mkoa unategemea kilimo, ufugaji, uchimbaji madini, uvunaji mazao ya maliasili, biashara, uzalishaji viwandani, utalii na ajira katika taasisi za Serikali na sekta binafsi. Hadi Kufikia mwaka 2015 kabla ya Mkoa kugawanywa na kuwa mikoa miwili ya Mbeya na Songwe, Mkoa wa Mbeya ulikuwa unachangia asilimia 7.4 kwenye Pato la Taifa ukiwa ni mkoa wa tatu baada ya Dar es Salaam na Mwanza. Hata baada ya kugawanywa, Mkoa wa Mbeya umeendelea kufanya vizuri ambapo hadi sasa Pato la Mkoa kwa mwaka 2016 lilifikia Sh. Trilioni 5.832, wastani wa Pato la mtu kwa mwaka 2016 ni Sh. 3,097,049.00 na Mkoa unachangia 5.62% ya Pato la Taifa ukiwa ukiwa ni Mkoa wa Pili baada ya Dar es Salaam.

Mhe Makalla amesema kuwa Mkoa wa Mbeya una jumla ya jumla ya viwanda 1,682, kati ya hivyo vikubwa ni 10 ambavyo ni Mbeya cement, PEPSI, Mbeya Breweries Co. Ltd, Coca cola Kwanza, Marmo E. Granito Mines (T) Ltd, Wakulima Tea Company, Katumba Tea Company, City Coffee, Tol Gases na Kapunga Rice Mills na viwanda vidogo 1,625 na viwanda vya kati ni 20. 

Aidha, Mkoa umeainisha minyororo ya thamani (value chains) za kuendelezwa ambayo ni alizeti, mahindi, viazi mviringo, maparachichi, mpunga, michichikichi, kakao, kahawa na maziwa na Matokeo chanya yameanza kuonekana. Kwa mfano, tayari tumeanzisha Kongani (clusters) ya alizeti yenye viwanda 41, Kongani ya Mpunga yenye viwanda 30, Kongani ya chakula cha mifugo yenye viwanda 3 katika Wilaya ya Mbeya. Aidha, tumeanzisha Kongani ya Mpunga maeneo ya Igurusi na Ubaruku Wilayani Mbarali yenye viwanda 17 na Kongani ya alizeti Chunya yenye viwanda 19, hivyo kufanya jumla ya Kongani za 3 zenye jumla ya viwanda 107 vya kuongeza thamani ya mazao.

Naibu Spika, Dr. Tulia Ackson Mkoa Mkoa una fursa za kipekee za vivutio vya utalii. Fursa za Utalii zilizopo ni pamoja kuwepo kwa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Hifadhi ya Taifa Kitulo, Hifadhi ya Mlima Asilia Rungwe, Pori la Akiba la Mpanga - Kipengere, Mapori ya Uwindaji Wilayani Chunya, Ziwa Ngosi Wilaya za Rungwe na Mbeya, Fukwe za Ziwa Nyasa na Kumbukumbu za Kihistoria. Fursa nyingine ni ujenzi wa Mahoteli, Migahawa ya kisasa na Maduka (shopping centres)

Dr. Ackson amesema kuwa Mkoa wa Mbeya uko katika eneo la kimkati kwa uwekezaji wa aina zote. Nimeeleza mafanikio yaliyopatikana kiuchumi. Maeneo ya kimkakati ya uwekezaji yameendelea kujengewa miundombinu muhimu inayochochea ukuaji wa sekta hasa kilimo ili kupata malighafi za viwanda

Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Kanda Bw Rupia amesema kuwa pamoja na hatua mbalimbali zilizofikiwa katika uwekezaji, bado kuna fursa kubwa ya kupanua uwekezaji katika Mkoa wetu wa Mbeya hususan katika sekta za kilimo, viwanda, utalii na madini. Malengo ya Kongamano letu la leo ni kuhamasisha, kukuza na kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo katika Mkoa, chini ya Kauli Mbiu ya “Uwekezaji katika Sekta ya Viwanda kwa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Mkoa Wa Mbeya”.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA IMES

    April 29, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YARIDHISHWA NA MAJIBU YA WADAU KUHUSU MAPENDEKEZO UGAWAJI WA JIMBO LA MBEYA MJINI.

    April 25, 2025
  • DKT. HOMERA AAGIZA MRADI KUKAMILIKA HARAKA IWEZEKANAVYO ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA

    April 14, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa