• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kituo cha Forodha chatakiwa Kuongeza Kasi ya Kukusanya Mapato

Imetumwa : September 10th, 2018

Mhe Mkuu wa Mkoa kukitaka kituo cha forodha cha Kasumulu  kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato na kusema jambo hili linawezekana kama taasisi zote zitafanya kazi kwa pamoja ili kubadilishana ujuzi katika maeneo yao.

Mhe.Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo leo Wilayani Kyela alipokuwa akiongea na watumishi mbalimbali wa halmashauri na taasisi za umma kwenye ziara ya kujitambulisha.

Ameitaka mamlaka ya forodha kukaribisha mawazo tofauti ya jinsi ya kutanua uwezo wa ukusanyaji wa mapato kwa kushirikisha mawazo mapya kutoka kwenye mamlaka nyingine ikiwa pamoja na wananchi wa eneo husika.

Mhe Chalamila ameitaka mamlaka hiyo pia kusimamia ulinzi na usalama wa mpaka kwa kuimarisha ulinzi na watu wajue kuwa mpaka unalindwa  kwani eneo hilo ni rahisi kupitika kwa wahamiaji haramu na magengo.

“kuna baadhi ya watumishi sio waadilifu katika kusimamia ulinzi wa mipaka lakini na walio waadilifu wanaitwa “wanoko”. Ni bora kuitwa “mnoko” kwa kusimamia sheria na kanuni za nchi kuliko kupendwa kwa kuvunja sheria na taratibu za Serikali” alifafanua Mkuu wa Mkoa.

Kamanda wa Polisi Mkoa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ulrich Matei  amewataka watumishi wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa kushirikiana kwa sababu mpaka huo umekuwa ukitumika sana kwa njia za panya kupitishia magendo, dawa za kulevya pamoja na wahamiaji haramu.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi Matei amewataka pia kuangalia ulinzi na usalama wa bidhaa zinazotoka na kuingia katika mpaka huo ili kujua madhara yake na kuhakikisha wanafunga njia zote za panya zinazotumiwa na wafanyabiashara kupitisha magendo hayo. 

Katika Mkutano wa hadhara Mkuu wa Mkoa ameagiza halmashauri kumtoa wakala anayesimamia utozaji wa mapato katika geti la mpaka wa Kasumulu na kazi hiyo isimamiwe na halmashauri baada ya kuona Serikali inapoteza mapato mengi kwenye geti hilo.

Mkuu  wa Mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila amewataka watumishi wa umma kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi na kutokuwa sehemu ya ushabiki wa kisiasa  kwa kupotosha jamii bali wawe mabalozi wazuri wa kutafsiri agenda za serikali katika kutekeleza dhana ya uwajibikaji katika maeneo yao ya kazi.

Amefafanua kuwa mtumishi wa umma hatakiwi kuwa sehemu ya vyama vya siasa kwa kuwa anaongozwa na kanuni, sheria na taratibu ambavyo vimemnyang’anya uwezo wa kuipinga serikali badala yake kuwa mshauri wa serikali katika shughuli za maendeleo.

“kama mtumishi wa umma hawezi kuelewa misingi ya utumishi wa umma akae pembeni kwa sababu hakuna demokrasia isiyodhibitiwa na sheria. Sheria za utumishi zipo kwa ajili ya kuwaongoza katika utendaji kazi wao ili kuepuka mihemko ya kisiasa” amesema Mkuu wa Mkoa.

Aidha, Mhe Chalamila amewataka watumishi wa umma kuwa waadilifu na kutumia vizuri mamlaka waliopewa na kutokuwa chanzo cha kuongeza malalamiko ya wananchi kwa Serikali bali wametakiwa kutoa huduma bora kwa kuangalia sera na agenda ya nchi kwa sasa.

Amewataka Maafisa mipango na biashara kujitafakari wanaisaidia vipi halmashauri yao na kuagiza wataalamu hao kuwa wabunifu kwa kuandika maandiko  ya kutengeneza vitega uchumi vinavyoweza kusaidia na kuiongezea halmashauri mapato ya ndani katika sekta za afya, elimu, viwanda na utalii.

Katika ziara hiyo Mhe Mkuu wa Mkoa ameongozana na Katibu Tawala wa Mkoa Bibi Mariam Mtunguja ambaye amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa ushirikiano na kusema kuwa wataalamu wa kiutendaji ndio wasaidizi wakuu wa Mkuu wa Mkoa katika kutekeleza majukumu ya maendeleo katika mkoa na hivyo ni muhimu kuwa na ushirikiano wa karibu katika utendaji kazi.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • RC DKT. HOMERA AKUTANA NA MABALOZI WA NCHI NNE AFRIKA

    May 26, 2025
  • "WAFUNDISHENI PIA ULAJI WA LISHE WATU MAOFISINI" - RC DKT. HOMERA

    May 26, 2025
  • FISTULA INATIBIKA, MATIBABU NI BURE, KARIBU UHUDUMIWE - DKT. HOMERA

    May 19, 2025
  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa