• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
      • Maji
      • Huduma ya Menejimenti ya Serikali za mitaa
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Menejimenti ya Serikali za mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mbeya Regional Commissioner Urgue the City Council to Accelerate Construction of Classes

Imetumwa : December 6th, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Amos Makalla ameongoza kikao kazi katika Halmashauri ya Jiji  la Mbeya kwa lengo la kuhamasisha upatikanaji wa fedha kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa baadhi ya madarasa katika shule zilizopo Halmashauri ya Jiji Mbeya.

Akifungua kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Mbeya alieleza dhumuni la kukutana kwa umoja huo lengo likiwa uhamasishaji ili kuwesheza watoto waliokosa shule kutokana na uhaba wa madarasa wanaanza shule ifikapo januari 09 mwaka ujao.

Mh.Makalla alitoa pongezi kwa kazi nzuri iliyofanyika ya ukamilishwaji wa madawati na ukarabati wa shule ya Sekondari Iyunga alisema “Kama tuliweza kukamilisha madawati na kukarabati shule iliyoinguabasi kukamilisha madarasa haya kuminaamini ni kazi ndogo na tutaiwezatukifanya kwa ushirikiano”

Pia aliwataka waratibu wa Elimu kuhakikisha wanashirikiana na Wataalamu toka Halmashauri ya Jiji ili kuhakikisha kazi inafanyikanakumalizika kwa wakati. Aliwataka wajumbe wa Bodi za Shule,Waratibu wa Elimu kata na  Kamati ya Elimu kuhakikisha wanasimamia nidhamu katika mashule ili kusaidia kizazi kijacho.

Akitoa Msisitizo wa shughuli hiyo Meya wa Halmashauri wa Jiji la Mbeya Mheshimiwa David Mwashilindi alizungumza kwa niaba ya madiwani nakusema atahakikishawa nakuwa mabaloz iwazuri kwa wananchi ili kuwezesha upatikanaji wa fedha ili kuharakisha zoezi hilo nakuwezesha wanafunzi kuingia mashuleni kwa wakati.

Nae Mkurugenzi wa Jiji NduguZ.Nachoa alisema Halmashauri ya Jiji imepang kutoa  kiasi cha shilingi milioni mbili kwa kila kata zilizo na upungufu wa madarasa ili kuwezesha zoezi hilo kuanza mara moja.

Kikao hicho kilihudhuriwa na  Mkuu wa Wilaya,Madiwani, Mkurugenzi wa Jiji ,Katibu Tawala wa Wilaya, Wakuu wa Idara na Vitengo, Wakuu wa Shule za Sekondari,Wakuu wa bodi za Shule,Waratibu wa Elimu Kata pamoja na Watendaji wa Mitaa kilichofanyika tarehe 6 Disemba 2016 katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji.

Halmashauri ya Jiji inajumla ya shule za sekondari  54 zikiwepo 31 za serikali na 23 za binafsi. Kwa mwaka 2016 jumla ya wanafunzi waliofanya mtihani wakumaliza elimu ya msingi ni 9,450 waliofaulu ni 6,613 kati ya hao waliochaguliwa kujiunga na shule za bweni ni 16, waliochaguliwa kujiunga na shule za kutwa ni 6,245 waliobaki kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa ni 352.

Kati ya hawa ambao hawakupata nafasi kutokana na uhaba wa madarasa ni kutoka shule za sekondari 8 ambazo ni Sekondari ya Sinde, Sekondari ya Ihanga ,Sekondari ya Iyela, Serikali ya Mwakibete, Sekondari ya Mponja, Sekondari ya Uyole, Sekondari ya Itezi na Sekondari ya Lyoto. Mahitaji ya madarasa kwa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza 2017 ni madarasa 166.Aidha madarasa yaliyopo ni 156 na kuwa na upungufu wa madarasa 10.

Matangazo

  • Fomu za Maelekezo kwa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano 2021 Shule za Mkoa wa Mbeya (Joining Instructions) June 07, 2021
  • Matokeo ya Kidato cha Sita 2020 August 21, 2020
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza 2021 Mkoa wa Mbeya. December 18, 2020
  • Uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji March 11, 2021
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • Katibu Mkuu Dkt. Jingu: Jamii ipewe elimu kuhusu Anwani za Makazi

    May 18, 2022
  • DKT. JINGU APONGEZA ZOEZI LA ANWANI ZA MAKAZI MKOANI MBEYA

    May 17, 2022
  • Waziri Nape aupongeza Mkoa wa Mbeya katika zoezi la Anwani za Makazi

    May 13, 2022
  • Rc Homera atatua mgogoro wa Ardhi uliodumu kwa miaka miwili

    May 13, 2022
  • Tazama Zaidi

Video

RC Atoa Onyo Kuelekea Uchaguzi
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Ajira

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Uzunguni Road

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025 2503034

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2019 Mbeya Region . All rights reserved.