• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Uchumi wa Mkoa wa Mbeya Unaendelea Kuimarika" RC Makalla

Imetumwa : November 23rd, 2017

KMkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amesema kuwa Uchumi wa Mkoa umeendelea kuimarika ambapo ambapo hadi sasa Pato la Mkoa kwa mwaka 2016 lilifikia Sh. Trilioni 5.832

Akiongea katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) Mhe Makalla amesema wastani wa Pato la mtu kwa mwaka 2016 ni Sh. 3,097,049.00 ambapo  Mkoa unachangia 5.62% ya Pato la Taifa ukiwa ni Mkoa wa Pili baada ya Dar es Salaam.

Mhe Makalla amesema kuwa Mkoa unatekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambayo inalenga kulifikisha Taifa kwenye uchumi wa kati ambao kwa sehemu kubwa utakuwa ni uchumi wa viwanda.

“ Mipango ya Serikali ya kufikia lengo hilo ni pamoja na utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 - 2020/21 ambao Serikali ya Awamu ya Tano imeamua uwe na dhima ya Kujenga Uchumi wa Viwanda ili Kuchochea Mageuzi ya Kiuchumi na Maendeleo ya Watu (Nurturing Industrialisation for Economic Transformation and Human Development).” Mhe Makalla

Naye Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uwezeshaji Bw. Enock Nyasebwa amesema kuwa Serikali inatekeleza Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mwaka 2004. Madhumuni ya Sera ni kuwashirikisha kikamilifu wananchi katika shughuli za uchumi. Sera ya Uwezeshaji inajumuisha wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyakazi na wafanyabiashara katika sekta mbalimbali na makundi mengine.

Bw. Nyasebwa amesema hadi sasa Mkoa umeanzisha madawati ya Uwezeshaji Wananchi katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri yanayoratibu shughulizi za kuwawezesha wananchi kuhusu mitaji, stadi za biashara, masoko, miundombinu ya kiuchumi, ushirika na ardhi. Aidha, Madawati ya Uwezeshaji Wanawake kiuchumi yameanzishwa katika Halmashauri za  Kyela, Rugwe, Mbeya Jiji, Mbeya na Chunya

“Mkoa unaendelea kuyatumia madawati haya kuwafikia wananchi taarifa muhimu kuhusu biashara na uwekezaji hususani ushiriki katika uanzishaji Viwanda Vidogo ili kufikia Uchumi wa kati kwa kauli Mbiu ya Mkoa wetu, Viwanda vyetu, Wilaya Yetu Viwanda Vyetu, Kata yetu viwanda vyetu, kijiji/mtaa wetu viwanda vyetu, kaya yetu viwanda vyetu.” Bw. Nyasebwa

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA IMES

    April 29, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YARIDHISHWA NA MAJIBU YA WADAU KUHUSU MAPENDEKEZO UGAWAJI WA JIMBO LA MBEYA MJINI.

    April 25, 2025
  • DKT. HOMERA AAGIZA MRADI KUKAMILIKA HARAKA IWEZEKANAVYO ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA

    April 14, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa