• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mkuu wa Mkoa asikitishwa na Matumizi Mabaya ya Fedha

Imetumwa : September 26th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila amesikitishwa na matumizi mabaya ya fedha katika ujenzi wa mradi wa bwawa la Lwanyo na kuishauri Wizara ya Maji kuwachukulia hatua za kinidhamu wale wote waliohusika katika ujenzi wa mradi huo.

Mhe. Chalamila ameyasema hayo leo tarehe 25 Semptemba, 2018 wakati akikagua mradi wa maji wa bwawa la Lwanyo katika ziara yake ya kikazi Wilaya ya Mbarali kukagua shughuli za maendeleo na kutatua kero za wananchi.

Amesema kuwa anaishauri wizara kwa sababu mradi huo wakati unajengwa fedha zilikuwa zinapita kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji kuja Ofisi ya Umwagiliaji Kanda ya Mbeya ambao ndio walikuwa wanasimamia ujenzi wa mradi huo.

 “Ushauri wangu kwa Mhe Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa ni kuwakamata wale wote waliohusika na ujenzi wa mradi kwa sababu mradi huu umetengenezwa na viongozi waliokosa uadilifu, wala rushwa na wasio na mapenzi mema na nchi yetu” Amesema Mhe. Chalamila.

Amesema kuwa inasikitisha kuona mradi umetumia zaidi ya shilingi bilioni 3.07 bado haujakamilika na ofisi ya umwagiliaji kanda wanaomba fedha nyingine za kwenda kumalizia mradi huo wakati fedha iliyokwisha kutumika na thamani ya mradi haviendani.

Kazi ya ujenzi wa  bwawa la Lwanyo ilifanywa na mkandarasi M/s Boimanda Modern Construction Co kwa gharama ya shilingi bilioni 2,951,363,153.70 chini ya usimamizi wa Ofisi ya Mhandisi wa Umwagiliaji Kanda ya Mbeya lakini mpaka kufikia tarehe 15 Disemba, 2013 gharama zilifikia shilingi bilioni 3.077,220,613.21 kutokana na changamoto zilizojitokeza wakati wa ujenzi ikiwemo ya uvujaji wa bwawa kwa sababu ya mapungufu ya uchunguzi wa udongo ardhi na miamba (Geotechnical Investigation Study).

Aidha, Mhe Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila amepata fursa ya kutembelea mashamba makubwa ya wawekezaji ya Kapunga Rice Project na Highlands Estate na kufurahishwa na namna makampuni hayo yanavyojitolea kuchangia shughuli za maendeleo katika maeneo yao na kuwaomba kuendelea na hamasa hiyo hasa katika kufanikisha agenda kuu ya Mkoa wa Mbeya ya kujenga Zahanati kila kijiji ifikapo mwaka 2020.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA IMES

    April 29, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YARIDHISHWA NA MAJIBU YA WADAU KUHUSU MAPENDEKEZO UGAWAJI WA JIMBO LA MBEYA MJINI.

    April 25, 2025
  • DKT. HOMERA AAGIZA MRADI KUKAMILIKA HARAKA IWEZEKANAVYO ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA

    April 14, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa