Mti huu ni aina ya Mvule na unapatikana masoko katika wilaya ya rungwe, mti huu ni mkubwa kiasi kwamba ili kuweza kuuzunguka wote unahitaji watu kuanzia nane waliounganisha mikono. ukiupima una futi 39 katika kimo cha juu kidogo lakini una futi 43 chini kabisa.
Wenyeji wa eneo lenye mti huu wanasema kuwa mti ni wa kale sana kiasi kwamba hawakumbuki hasa ni wa miaka gani lakini walioweza kutunza angalau historia ni kuanzia karne ya 13 lakini nao waliukuta ukiwa mkubwa sana
Mnamo mwaka 1975 mti huu kwa mara ya kwanza ulidondosha tawi lake moja ambalo hata ukifika inaonyesha maana pana onekana ni wapi hasa lilikuwepo na inasemekana lilipoanguka ilikuwa kama tetemeko la ardhi kutokana na kishindo kilichotetemesha kijiji kile na vijiji jirani.
Katika tawi la kwanza kuna sehemu ya mti huu kutokana na kuwa njia ya kutolea maji ule utomvu wake wa muda mrefu umejikusanya na umefanya umbo lenye muonekano wa pembe hivyo wenyeji huita eneo lile LUPEMBE, sehemu hiyo yanadondoka maji tone moja moja kama yadondokavyo katika dripu na rangi ya maji hayo ni mekundu kiasi kwamba baadhi ya watu huamini kuwa ni damu iliyotumika kama mazindiko hapo zamani. lakini mwenyeji anasema kuanzia karne hiyo ya 13 wanavyoelezwa hakukuwa na matambiko yoyote labda kabla ya karne hiyo, na asilimia kubwa ya matawi ya mti huu yana nyuki,karibu utembelee maeneo haya uweze kujifunza mengi
Chanzo. Mbeya Home of Tourism
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa