• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

RC Homera Ataka 90% za Ufaulu

Imetumwa : May 31st, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Homera ameiagiza Halmashauri za Mkoa wa Mbeya kunyanyua kiwango cha ufaulu kwenye shule za msingi na sekondari mpaka kufikia angalau asilimia tisini kwa vile jambo hilo linawezekana.

Mheshimiwa Juma Homera ameyazungumza hayo leo hii kwenye kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mkapa ambapo amewaagiza kuinua kiwango hicho cha ufaulu na kufikia angalau asilimia tisini (90%) kutoka kile cha awali cha asilimia 78% kwa shule za sekondari na asilimia (89%) kwa shule za msingi.

Aidha katika kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinaongezeaka na kufikia lengo la asilimia tisini Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera ameweka bayana baadhi ya mikakati Ikiwemo kuandaa makambi kwa kila shule  kwa ajili ya wanafunzi kujisomea na kufanya majaribio wiki mbili au tatu kabla ya mitihani ya mwisho, wanafunzi kufanya mitihani ya majaribio mara tatu kwa mwaka ambapo Halmashauri inatakiwa kugharamia zoezi hilo.

Pamoja na hayo Mkuu huyo wa Mkoa amezitaka Halmashauri zote mkoani humo kuunda dawati la kushughulikia kero za walimu na kuwasaidia kupata stahiki zao kwa wakati kwani kufanya hivyo kutawapa hali ya kufanya kazi kwa weledi na hatimaye kufanikisha kuinua kiwango cha ufaulu cha sasa nakufikia lengo la asilimia tisini linalotazamiwa.  

Kwa upande mwingine Mheshimiwa Homera amewaagiza waratibu elimu kata  kutembelea na kukagua maendeleo ya elimu kwenye kata zao ili kubaini changamoto na uzembe unaopelekea kukwamisha kiwango cha ufaulu kuongezeka na watakaobainika kufanya vibaya wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Zuberi Homera ambaye ana wiki ya pili sasa tangu alipoapishwa amendelea kuwasisitiza watumishi hasa wakuu wa Idara mbalimbali katika Halmashauri za mkoa wa Mbeya kuwa wabunifu kwa vile ubunifu unasaidia kutatua changamoto na kupiga hatua kwenye maendeleo.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA IMES

    April 29, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YARIDHISHWA NA MAJIBU YA WADAU KUHUSU MAPENDEKEZO UGAWAJI WA JIMBO LA MBEYA MJINI.

    April 25, 2025
  • DKT. HOMERA AAGIZA MRADI KUKAMILIKA HARAKA IWEZEKANAVYO ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA

    April 14, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa