Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Juma Zuberi Homera ametoa maelekezo kwa wakuu wote wa Wilaya ndani ya mkoa wa Mbeya kushughulikia swala la kupanda kwa bei za bidhaa hususani zinazozalishwa ndani ya nchi.
Kauli hii ya Mkuu wa Mkoa imetolewa mapema siku ya leo mara baada ya Waziri mkuu Mh.Kassim Majaliwa Majaliwa kutoa maagizo hayo leo wakati akizungumza na viongozi wa Mikoa na Wilaya kuhusu maendeleo na maandalizi ya Sensa ya watu na Makazi kwenye kikao kazi alichokiendesha kwa njia ya mtandao (video Conference) kutokea ofisi kwake Mlimwa, jijini Dodoma.
Uzunguni Road
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025 2503034
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Copyright ©2019 Mbeya Region . All rights reserved.