• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

TANAPA kusaidia Miradi ya Maendeleo ya Vijiji Zilivyo Pakana na Hifadhi

Imetumwa : March 13th, 2020

Faida zinazopatikana kutokana na uhifadhi zinarudi kwa wananchi kupitia shughuli za maendelo – Lihiru

Hayo yamesemwa na mjumbe wa timu maalumu ya kutoa elimu ya uhifadhi na ujirani mwema Mhifadhi kutoka Hifadhi ya Taifa kitulo Ndg. Agricola Lihiru alipokuwa akitoa elimu kuhusina na uhifadhi wa hifadhi za taifa pamoja na ujirani mwema siku ya tarehe 12/03/2020

Lihiru amesema kwamba zipo faida nyingi tunazoweza kuzipata kutoka kwenye uhifadhi ikiwemo kuendeleza miradi ya maendeleo iliyoibuliwa na wananchi kwa kuchangia asilimia 90 ya mradi na kuchangia kwenye mfuko wa taifa ili kusaidia shughuli za kimaendeleo.

Mhifadhi amebainisha baadhi ya miradi iliyofadhiliwa na Hifadhi ya Taifa za Tanzania (TANAPA) kuwa ni pamoja na ujenzi wa bwalo la shule ya sekondari ya Mawindi,  utengenezaji wa madawati katika shule ya msingi ya Luango, ujenzi wa vyumba vya madarasa Kata ya Igava pamoja na ujenzi wa  zahanati  ya Madibira.

Naye Afisa Ujirani Mwema kutoka Hifadhi ya Taifa ya Kitulo  Ndg Mollel Heriel ameweza kubainisha mambo mbalimbali ambayo hayaruhusiwi katika maeneo ya hifadhi kuwa ni pamoja na kutokufanya shughuli za kibinadamu kama kuwinda , kuingiza mifugo, kuweka makazi, kuchoma moto na mkaa kuwinda wanyama pori, kuvuna misitu,, uvuvi,  kuwinda , kuchimba madini na kuingia na silaha yoyote.

Aliongeza kuwa muingiliano wa wanyama wa kufugwa na wanyamapori inaharibu uasilia wa wanyama pori pamoja na muingiliano wa magonja kutoka kwa wanyama wa kufungwa kwenda kwa wanyama pori au wanyama pori kwenda kwa wanyama wa kufugwa majumbani

Muikolojia Kutoka Hifadhi ya Taifa Ruaha  Ndg Daniel Mathayo aliongeza kuwa kuna hifadhi 22 za taifa kwa sasa ambazo zinahifadhi wanyama pori na mazingira ambapo katika hifadhi hizo wananchi na wageni wanaruhusiwa kwenda kufanya utalii wa picha ambapo kwa mtanzania mtu mzima ni tsh. 5000 na mtoto ni 2000 vilevile inaruhusiwa kwenda kufanya matambiko kwa kibali maalumu ili waweze kupatiwa ulinzi.

Aliongeza kuwa TANAPA imeanzisha tuzo ya uhifadhi mazingira ambayo inashindanisha wananchi ambao wanafanya shughuli za uhifadhi wa mazingira kama watu binafsi, taasisi, vikundi na jumuiya za watumia maji ili kuimbarisha ujirani mwema, kuboresha mazingira na vyanzo vya maji, ambapo kwa sasa imeshafanyika kwa wilaya za Mbarali, Wangingombe, Makete, Mufindi na Kilolo na mwaka huu imeongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA IMES

    April 29, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YARIDHISHWA NA MAJIBU YA WADAU KUHUSU MAPENDEKEZO UGAWAJI WA JIMBO LA MBEYA MJINI.

    April 25, 2025
  • DKT. HOMERA AAGIZA MRADI KUKAMILIKA HARAKA IWEZEKANAVYO ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA

    April 14, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa