• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wakuu wa Idara watakiwa kuwa Wabunifu

Imetumwa : September 14th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Chalamila amewataka wakuu wa idara katika halmashauri kutambua na kuelewa mipaka ya majukumu ya kila mmoja, kuibua mapendekezo yanayoweza kuibua miradi mbalimbali ya maendeleo na uwekezaji wa viwanda kwa kutumia rasilimali zetu na kuacha kuilalamikia serikali.

Mh. Albert Chalamila leo Septemba 12, 2018  ameendelea na ziara yake Wilaya ya Rungwe ambapo alipata nafasi ya kuongea na watumishi wa umma na kuwataka wakuu wa idara kuwa wabunifu ili  kuleta tija kwa serikali katika maeneo yao.

“ na mimi nimesema kuwa mkuu wa idara au mtumishi mwingine yeyote asiye mkuu wa idara atakayeandika andiko lake vizuri, mimi kila andiko nitampa shilingi 1,000,000 andiko kuhusu maboresho ya shule, maji, zahanati au viwanda” Amesema Chalamila.

Mhe Chalamila amesema Wilaya ya  Rungwe inaongoza kwa kuwa wazalishaji wakubwa wa mazao ya kilimo lakini mpaka leo hakuna mpango mkakati wowote wa uwekezaji wa viwanda na kuwataka wataalamu kuacha kubishana kuhusu masuala ya wawekezaji kwa sababu wanalipotezea muelekeo taifa.

“Nimeambiwa hapa kuna Heifer International na ASAS Group lakini hakuna kinachoendelea, Kuna matatizo Rungwe na kama tutaendelea kubishana sisi wataalamu kwa maslahi yetu wenyewe tunalipotezea taifa muelekeo. Ni kitendo cha fedheha na aibu unapokuta mwekezaji analia kwamba ameombwa rushwa ndipo aje awekeze” Amesema Chalamila.

Amefafanua kuwa inashangaza kuona mikoa mikubwa inayozalisha chakula kwa wingi haijawahi kuwa na mpango wa kuwa na kiwanda kikubwa cha mbolea au viwanda vya kuongeza thamani mazao na kufanya mpaka leo wakulima kuendelea kusafirisha ndizi na viazi kwenye magari badala ya kufanya ‘package’ na kusafirisha kwa kutumia usafiri wa ndege na watu wakala chakula kilikikiwa katika hali ya upya.

Aidha, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila amepata fursa ya kutembelea na kukagua ujenzi na ukarabati wa chuo cha Ualimu cha Mpuguso unaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 9.6 ambao unajengwa na Wakandarasi wawili wa Lukolo Company Limited na Salem Construction Limited.

Mkataba wa Lukolo Company Limited unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.8 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, maktaba, maabara na ukarabati wa mabweni mawili na vyoo na Salem Construction Limited ambaye ana mradi wa ujenzi wa mabweni mawili, nyumba nne za watumishi, ukarabati wa nyumba 4, kujenga tanki la kuhifadhia maji na kujenga nyumba ya huhifadhia maji kwa mkataba wa shilingi billion 5.7.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • RC DKT. HOMERA AKUTANA NA MABALOZI WA NCHI NNE AFRIKA

    May 26, 2025
  • "WAFUNDISHENI PIA ULAJI WA LISHE WATU MAOFISINI" - RC DKT. HOMERA

    May 26, 2025
  • FISTULA INATIBIKA, MATIBABU NI BURE, KARIBU UHUDUMIWE - DKT. HOMERA

    May 19, 2025
  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa