Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera ameongoza kikao cha Tathmini ya lishe mkoani Mbeya kilichofanyika mapema leo katika ukumbi wa Mkapa jiji Ia Mbeya ikiwa ni utekelezaji wa Agizo la Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan. Katika kikao hicho wajumbe walipata nafasi ya kujadili kwa kina hali ya utekelezaji wa Afua za lishe, Mikakati ya namna ya kuboresha Lishe ikiwa ni pamoja na Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya kutia saini Mkataba wa utekelezaji wa Afua za Lishe.
Mkuu wa Mkoa amewaagiza watendaji wote katika sekta ya Afya kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ili kujenga jamii ya watu wenye afya njema inayoendana na kasi ya ujenzi wa Tanzania ya Viwanda. Amewaagiza pia Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanatekeleza kikamilifu makubaliano ya mkataba waliosaini wa Utekelezaji wa Afua za Lishe ikiwa ni pamoja na kuhakikisha tathmini inafanyika mara kwa mara ili kupima kiwango cha utekelezaji ambacho Wilaya imefikia.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa