• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wakuu wa Wilaya watakiwa Kutimiza Wajibu Wao

Imetumwa : January 31st, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mbeya Mhe Amos Makalla ameweka kikaangoni Wakuu wa Wilaya baada ya kuwaagiza kuandika barua za kujieleza kwa kushindwa kutekeleza agizo la Serikali la kufikia asilimia 100 ya uwekaji alama mifugo na kwamba wasipende kumjaribu katika utendaji wa kazi.

Makalla ametoa agizo hilo alipokutana na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wenyeviti wa Halmashauri  katika ukumbi wa mikutano akisisitizi kuwa agizo hilo ni la Wizara ya Kilimo na Mifugo katika kufuatilia utekelezaji wa zoezi hilo.

Mhe. Makalla amesema kuwa ifikapo Februari Mosi barua hizo ziwe zimewasilishwa ofisini kwake ili ziweze kuambatanishwa na utekelezaji wa zoezi la uwekaji wa alama mifugo na kuwasilisha wizarani haraka iwezekanavyo.

Aidha, amewatahadharisha Wakuu wa Wilaya kutowahusisha Wakurugenzi wa Halmashauri kuhusu kukwamisha zoezi hilo kwa kuwa jukumu hilo walikabidhiwa wao ili kufikikia malengo waliyopewa na Serikali.

“  Ninawaomba katika hizo barua msiwatwishe mizigo Wakurugenzi kuwa ndio kikwazo, Mimi nilizindua zoezi la uwekaji alama mifugo kila Wilaya toka Mwaka Jana lakini Wakuu wa Wilaya mmelipuuza" Mhe Makalla.

Alisema kuwa Wakuu wa Wilaya wasipende kumjaribu katika utendaji wa kazi na kwamba kila mtu ana wajibu wa kulinda kibarua chake na ufike wakati wa kufanya kazi kwa kujituma na si mazoea kwa Serikali hii ya Awamu ya Tano.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa Mama Mariam Mtunguja amesema kuwa Watendaji wa Serikali wanapaswa kutambua majukumu yao na maagizo kutoka ngazi za juu na kwamba usifike wakati wa kukumbushwa majukumu yao na kuwataka kila Mtendaji atimize Wajibu wake.

Mama Mtunguja amesema kuwa wanapaswa kumtumia vizuri Mkuu wa Mkoa katika uwajibikaji na utekelezaji wa majukumu kwa kuwa anatoa ushirikiano mkubwa na si kumlazimisha kufanya maamuzi magumu.

Aidha amefafanua kuwa katika Halmashauri zote Mbeya Jiji imefanya vizuri kwa kufikia asilimia 100 wakati Mbarali ina 83, Kyela 82, Mbeya DC 81, Busokelo 75 na Rungwe kushika nafasi mwisho kwa asilimia 27 wakati ndio inayozalisha maziwa kwa wingi kutoka Mkoa wa Mbeya


Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • RC DKT. HOMERA AKUTANA NA MABALOZI WA NCHI NNE AFRIKA

    May 26, 2025
  • "WAFUNDISHENI PIA ULAJI WA LISHE WATU MAOFISINI" - RC DKT. HOMERA

    May 26, 2025
  • FISTULA INATIBIKA, MATIBABU NI BURE, KARIBU UHUDUMIWE - DKT. HOMERA

    May 19, 2025
  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa