• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Waliovamia Hifadhi na Mapori ya Akiba Watakiwa Kuhama

Imetumwa : August 29th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amewaagiza wananchi  wa Mkoa wa Mbeya ambao wamevamia hifadhi na mapori ya akiba kuondoka kwa hiari katika maeneo hayo kama walivyokubaliana kabla Serikali haijachukua hatua za kuwaondoa ili kulinda uharibifu wa mazingira.

Akizungumza kwenye kwenye kikao maalum cha baraza la Madiwani Chunya Mhe Makalla amewataka wananchi wote waliovamia hifadhi, mapori na vyanzo vya maji wahame kwa hiari ndani ya kipindi cha wiki tatu (3) kabla Serikali ya Mkoa haijaanza kampeni ya kuwaondoa katika maeneo hayo

“Natoa agizo kwa Kamati za Ulinzi na Usalama Kila Wilaya kukagua utekelezaji wa agizo hili kuanzia Septemba 20, 2017 na kwa wale ambao watakaidi agizo hili hatua stahiki zitachukuliwa kwani wananchi walivamia maeneo hayo wamekaidi kuhama kwa muda mrefu na niliamua kuwapa nafasi zaidi pasipo kutii agizo hilo na wananchi hao waliovamia hifadhi wasajiliwe katika vijiji vilivyopo katika vijiji vingine .”  Mhe. Makalla

Mhe Makalla amesema kutakuwa na operasheni za kushtukiza katika hifadhi na mapori yote ya akiba kila mara  ili    kuangalia kama kuna shughuli zozote za kibinadamu zinazoendelea katika maeneo hayo. Lengo kubwa ni kulinda vyanzo vya maji na uhifadhi wa mazingira.

Aidha, Amesema kuwa Katika hatua nyingine Mhe Makalla amewataka wananchi kuendelea kupanda miti kwa wingi ili kuepuka hali ya Ukame ambao utapelekea kuwepo kwa Jangwa katika maeneo yao na kuwa na utamaduni wa kupanda miti ya vivuli na matunda katika makazi na vyanzo vya maji.

Mhe Makalla amewataka Wakuu wa Wilaya zote kukaa na uongozi wa Vijiji vyote vilivyopo katika safu za milima na kuangalia jinsi gani watazuia tabia ya baadhi ya wananchi kuchoma misitu hovyo na kuharibu mazingira.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA IMES

    April 29, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YARIDHISHWA NA MAJIBU YA WADAU KUHUSU MAPENDEKEZO UGAWAJI WA JIMBO LA MBEYA MJINI.

    April 25, 2025
  • DKT. HOMERA AAGIZA MRADI KUKAMILIKA HARAKA IWEZEKANAVYO ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA

    April 14, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa