• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wananchi Watakiwa Kulinda Miundombinu ya Maji

Imetumwa : March 23rd, 2021

Mkuu wa Mkuu wa Mbeya Mhe Albert Chalamila amewataka wananchi wake kuwa walinzi wa miundombinu katika miradi ya maji inayopelekwa katika maeneo yao huku wakitambua na kuzingatia kuwa, lengo la Serikali ni kuboresha maisha yao kwa kuwasogezea huduma.

Alisema hayo alipozungumza na wakazi wa kijiji cha Lugombo, kata ya Kandete katika Halmashauri ya  Busokelo wilayani Rungwe akiwa ziara ya kukagua mwendelezo wa ujenzi wa Mradi wa Maji wa Mwakaleli 1 Skimu ya Ndala unayotekelezwa kwa akaunti ya dharura.

Alisema kuwa kumekuwa na kasumba ya baadhi ya watu kuhujumu miundombinu ya miradi ya maji hatua inayorudisha nyuma jitihada za seikali kuwafikishia wananchi huduma bora za kijamii

“ Yapo baadhi ya maeneo hususani yaliyo na wafugaji, watu wanaotumia mishale kutoboa mabomba yanayopitisha maji kupeleka kwa wananchi ili wanyweshe mifugo yao. Sasa kuna wakati tunafikiri  na wao tutumie mishale hiyo hiyo kuwatoboa ili tuwaulize kuna maumivu kiasi gani” alisema Mkuu wa Mkoa

Akaongeza “ Tutambue kuwa serikali imedhamiria wananchi kuondokana na tatizo la maji..Vyanzo vya maji tunavyo, lakini maji hatujayaweka vizuri ili yafike kwa wananchi, wapo watu wachache wanaotaka kutukwamisha: tuseme hapana” Chalamila

Awali, Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Usambazaji Maji Vijijini (RUWASA) Paul Kambona alisema, mwanzoni mradi huo katika skimu ya Ndala ulikuwa unatekelezwa na RUWASA kwa usimamizi wa wilaya baada ya mkandarasi kusuasua

Alisema Skimu ya Ndala ina vijiji vinane na mradi unatarajiwa kunufaisha wakazi 12,217. Hadi sasa ujenzi wa chanzo umekamilika na sasa shughuli inayoendelea ni uchimbaji mitaro kwa ajili ya kuanza kulaza mabomba.

Alizitaja changamoto zinazokwamisha mradi huo kuwa ni pamoja na ubovu wa barabara kuelekea mahali kilipo chanzo vha maji unaosababisha kushindwa kufikisha mabomba kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha wilayani hapa.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA IMES

    April 29, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YARIDHISHWA NA MAJIBU YA WADAU KUHUSU MAPENDEKEZO UGAWAJI WA JIMBO LA MBEYA MJINI.

    April 25, 2025
  • DKT. HOMERA AAGIZA MRADI KUKAMILIKA HARAKA IWEZEKANAVYO ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA

    April 14, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa