Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera amesema kuwa wanafunzi zaidi ya 5000 wote waliokosa sifa ya kujiunga katika Mfumo ulio rasmi wamewapangia katika vyuo mbalimbali ikiwa na lengo la kuondoa mfumuko wa watoto wa mitaani katika Mkoa wa Mbeya.
Wanafunzi waliokosa sifa za kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za serikali wamepatiwa fursa ya kujiunga na vyuo vya ufundi stadi (Veta) katika vituo mbali mbali hususan vinavyomilikiwa na watu binafsi.
Homera amesema kuwa katika kundi hilo pia wapo wanafunzi ambao watajiunga na elimu ya mfumo wa Memkwa kwa lengo la kuondokana na taifa kuwa na makundi ya watoto wa mitaani ajira katika umri mdogo .
Homera amesema hayo leo wakati akitoa taarifa ya masuala ya elimu kwa wanafunzi ambao hawajachaguliwa kidato cha kwanza 5,236 na mikakati ya mkoa ilivyojipanga kwa wanafunzi waliokosa nafasi.
Homera amesema kuwa katika mkoa wa mbeya 5,236 walipata madaraja B na E hawakuwa na sifa za kujiunga na elimu ya kidato cha kwanza katika shule za serikali walikaa na watalaam waliamua kuwapanga kwenye vyuo mbali mbali vya ufundi na elimu ya watu wazima.
Amesema sababu ya kuwapanga kwenye vyuo hivyo ni kutekeleza Ilani ya chama chama cha mapinduzi ya mwaka 2020 /2025 iliyolenga kuboresha ubora wa elimu hususani elimu ya ufundi ,mafunzo ya ufundi stadi hii ikiwa ni pamoja na utoaji elimu nje ya mfumo rasmi (MEMKWA)ili kuwawezesha walikosa sifa za mfumo rasmi kuweza kutimiza ndoto zao za kielimu.
Aidha Homera amesema kuwa kitu kingine kilichopelekea mkoa kufanya hivyo ni pamoja na kupunguza vijana wasio na kazi mitaani ambapo hugeuka kuwa wahalifu katika jamii mfano panya riad , nyuki .
Amesema ni vema watoto wote 5,236 waliokosa fursa za kujiunga na kidato cha kwanza wajiunge kwenye vyuo vilivyopo ndani ya mkoa wa Mbeya sababu nyingine ni kuongezeka kwa mzunguko wa fedha kwenye jamii ambapo wataongezeka mafundi umeme , wapishi ,na mafundi wengine muhimu watapatiwa elimu hiyo.
Amesema katika vyuo vilivyopo mkoani Mbeya kila chuo kimepewa idadi ya wananchi ambapo kwa Wilaya ya Kyela kuna vyuo 19 watachukuliwa wanafunzi 746, Busokelo wanafunzi 421, Chunya wanafunzi 80, Mbarali vyuo 7 .
Kwa Upande wa Mbeya Jiji wanafunzi 3,113 na Mbeya vijijini wanafunzi 1,634 na Rungwe wanafunzi 489 ambapo jumla ya vyuo vyote ni 52 hivyo kufanya idadi ya wanafunzi wote 5,236 waliokosa nafasi kupata nafasi za kujiunga na elimu ya ufundi.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa