• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Watumishi wa Umma Watakiwa Kutoa Taarifa Kwa Wananchi

Imetumwa : July 2nd, 2019

Na Esther Macha,Rungwe

SERIKALI Mkoani Mbeya imewataka watumishi wa umma kutoa taarifa sahihi kwa  wananchi za mapato na matumizi ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao kupitia mikutano ya hadhara na mbao za matangazo

Wananchi wakijua namna kodi zao zinavyotumika watapunguza malalamiko na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ambazo zinakuwa zinafanyika katika maeneo yao.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Albert Chalamila wakati kikao cha baraza la madiwani kilichokuwa kikijadili majibu ya hoja na mapendekezo ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG) kwa mwaka 2017/2018 kwa halmashauri za Wilaya ya Busokelo na Rungwe.

Aidha Chalamila aliwataka watumishi wa umma kuhakikisha kuwa wanasimamia fedha za umma na kutumika kwa maslahi ya umma na siyo maslahi ya mtu binafsi.

“Lakini pia ongezeni ukusanyaji wa mapato ya ndani na ni lazima yaendane na nidhamu ya matumizi na jukumu lenu ni kusimamia na kuhakikisha kuwa mapato yote yanayokusanywa kutoka kwenye vyanzo vya ndani na ruzuku ya serikali kuu yanatumika katika malengo yaliyokusudiwa”alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Hata hivyo Chalamila alisema ufuatiliaji wa mara kwa mara  ufanyike ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa na manunuzi yote ya umma yanayofanyika yana thamani ya fedha iliyotumika.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kikao hicho pia kilikuwa kinapitia utekelezaji wa mapendekezo ya CAG  kwa mwaka 2017/2018 na hoja ya miaka ya nyuma ili kuona mapungufu yaliyobainishwa kwa halmshauri ya Busokelo na jinsi yalivyoshughulikiwa na namna ilivyojipanga kwa kaguzi zijazo.

Akizungumzia kuhusu halmashauri ya wilaya Rungwe kupata hati isiyoridhisha kwa mwaka 2017/2018  Chalamila alisema zilizoanishwa na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali bbadhi ni  malipo yenye viambatisho pungufu sh. Mil.114,409,000,hati za malipo ambazo hazikuonekana kwenye ugaguzi sh.mil.8,645,000 pamoja na vitu vingine.

Kwa upande Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya ,Mariamu Mtunguja alisema kati ya wilaya tano za Mko wa mbeya wilaya ya Rungwe pekee ndo wametia doa kwa kupata hati isiyoridhisha kitendo hiki si kizuri kabisa.

“Aidha aliwataka viongozi wa halshauri ya wilaya Rungwe kuwa na ushirikiano  kwa wakaguzi wanapofika katika halmashauri zao na kwamba kama wanahitaji taarifa yeyote watoe kusiwepo na tabia ya kuficha taarifa.

Mkuu wa Wilaya Rungwe, Julius Charya alisema kwamba baada ya kufanyika ukaguzi halmashauri ilipata hati yenye mashaka na kuwa hali hiyo ilitokana na usimamizi hafifu kwenye miradi ya maendeleo iliyopita na kwamba ipo haja kwa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri kuchukua hatua kwa watendaji wasiowajibika na madiwani nao wawe wasimamizi wazuri.


Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA IMES

    April 29, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YARIDHISHWA NA MAJIBU YA WADAU KUHUSU MAPENDEKEZO UGAWAJI WA JIMBO LA MBEYA MJINI.

    April 25, 2025
  • DKT. HOMERA AAGIZA MRADI KUKAMILIKA HARAKA IWEZEKANAVYO ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA

    April 14, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa