TAARIFA YA USIMAMIZI MIRADI YA MAENDELEO
Katika mwaka 2017/2018 Mkoa wa Mbeya unayotekeleza Mpango wa kuendeleza Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGGOT), Mpango wa kuendeleza kilimo cha zao la korosho na Programu ya kuendeleza mazao ya Bustani. Katika msimu wa 2017/2018 Wilaya za Kyela, Chunya na Mbarali zimeotesha miche 132,440 ya korosho itakayopandwa katika eneo la hekta 1,892. Mkoa umepata kilo 946 za mbegu Korosho viriba vyeusi kilo 249 na matandazo kilo 78 kwa lengo hilo. Katika kuendeleza mazao ya bustani Mkoa kwa kushirikiana na TAHA na wadau wengine umefanikiwa kuunda vikundi 60 vyenye jumla ya wakulima 2,267 waliopatiwa mafunzo ya mbinu bora za uizalishaji, masoko na lishe.
1.1 Umwagiliaji
Mkoa unaendelea kuboresha miundombinu ya umwagiliaji ili kuongeza tija na matumizi bora ya rasilimali za maji. Mkoa una hekta 110,721 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Jumla ya hekta 51,046 zinamwagiliwa ikiwemo hekta 25,626 zilizoboreshwa na hekta 25,420 za asili. Aidha, katika kipindi cha 2016/2017 uboreshaji wa miundombinu uliendelea kufanyika kwenye skimu 6 katika Halmashauri ya Wilayani Mbarali (5) na Halmashauri ya Mbeya (1) kwa gharama ya shilingi 1,822,916,863. Hali ya utekelezaji wa miradi hiyo imeoneshwa katika Jedwali 1.
Jedwali Na.1: Hali ya Miradi ya Umwagiliaji
Na. |
Jina la Mradi
|
Jina la Mkandarasi |
Lengo la Mradi |
Gharama ya Mradi (Sh) |
Kazi Zilizofanyika |
1 |
Ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji Gwiri
|
Fair Classy Construction Ltd, S.L.P 5003, Morogoro kwa Mkataba Na. LGA/076/W/2016-2017/14
|
Ujenzi wa daraja na nguzo za mageti kwenye banio, vikamata mchanga 2, na Usakafia wa mifereji ya kati mita 350
|
249,028,085.00 |
Ujenzi wa daraja na nguzo za mageti kwenye banio, vikamata mchanga 2, na Usakafia wa mifereji mita 240 (Mfereji Mkuu mita 47 na Mfereji wa kati mita 193)
|
2 |
Ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji Uturo
|
IRA General Enterprise Co. Ltd S.L.P. 852, Mbeya kwa Mkataba LGA/076/W/2015-2016/13
|
Ujenzi wa mfereji mkuu mita 600
|
199,042,388.20 |
Ujenzi wa mfereji mkuu mita 600
|
3 |
Ujenzi wa Skimu za Umwagiliaji Uturo na Ukwavila
|
Classical Engineering Co. Ltd wa S.L.P. 4204 Mbeya kwa Mkataba Na. LGA/076/W/2015-2016/67
|
Kusakafia mfereji mkuu mita 500 wa skimu ya Uturo, na Ujenzi wa makalvati 15 kwenye barabara ya skimu ya Ukwavila.
|
145,022,000.00 |
Kusakafia mfereji mkuu mita 500 skimu ya Uturo, na ujenzi wa makalvati inaendelea.
|
4 |
Ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji Mwendamtitu
|
DryWall Building Construction Co. Ltd na JV APE Engineering Service Co. Lld S.L.P. 240, Iringa kwa Mkataba LGA/076/W/2015-2016/11
|
Ujenzi wa daraja na nguzo za mageti kwenye banio, Kichuja mchaga, Kuta za gabion, makalvati, Vigawa maji na vifolu, Tuta la mfereji mkuu na Usakafia wa mfereji mkuu mita 400
|
729,903,750.00 |
Ujenzi wa Kichuja mchaga, Kuta za gabion, Vigawa maji, Tuta la mfereji mkuu na Usakafia wa mfereji mkuu mita 400
|
5 |
Ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji Igomelo
|
Ms.KATAGAITO TRADERS CO. LTD, S.L.P. 735, TUKUYU- MBEYA kwa mkataba Na. LGA/076/W/2016-2017/12
|
Ukarabati wa banio na Usakafiaji wa mfereji mkuu mita 730
|
249,920,639.36 |
Usakafiaji wa mfereji mkuu mita 1,345
|
6 |
Ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji Mshewe
|
HAFRI TECH (T) LTD
|
Kusakafia mfereji mkuu mita 1250 na mfereji wa upili mita 400
|
250,000,000.00 |
Usakafiaji mfereji mkuu mita 200 na mfereji wa upili mita 400. Kazi iatakamilika mwishoni mwa mwezi Agosti, 2017
|
|
JUMLA KUU
|
1,822,916,863 |
|
Chanzo: Halmashauri ya Mbarali na Mbeya, 2018
1.2 Maghala
Jumla ya maghala 13 (Ilembo, Izyira, Ihombe, Idimi, Iwowo, Mlowo, Mbagala, Izumbwe, Igale, Njelenje, Isangala, Iwiji na Pashungu) katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya yalikarabatiwa chini ya Mfumo wa Stakabadhi ya Mazao Ghalani kwa zao la mahindi kwa gharama ya Shilingi 1,467,094,175.00. Ukarabati wa maghala haya umefikia wastani wa asilimia 96.
Katika skimu za umwagiliaji Mkoa ulilenga kujenga maghala 7 (Mbarali 5 na Kyela 2) kwa gharama ya shilingi 5,714,622,821.64. Maghala yote yamekamilika. Mpango wa Mkoa wa ujenzi/ukarabati wa maghala unalenga kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna na kuwaunganisha wakulima na mifumo ya masoko
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa