• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
      • Maji
      • Huduma ya Menejimenti ya Serikali za mitaa
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Menejimenti ya Serikali za mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mkoa wa Mbeya Wajiwekea Malengo ya Upandaji miti

Imetumwa : January 13th, 2021

Mkoa wa Mbeya umepanda miti 6,080,667  mwaka 2019/2020 sawa na asilimia 58 ya lengo lililowekwa kimkoa la kupanda miti 10,500,000 kwa mwaka.

Hayo yamesemwa na Ndugu Said Madito, Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti kimkoa iliyofanyika Wilaya ya Mbarali na kusema kuwa miti 4,424,092 ilistawi sawa na asilimia 73 ya miti yote iliyopandwa.

Madito amesema kuwa tangu mvua zimeanza kunyesha zaidi ya miti 102,799 imepandwa kwa kushirikiana Viongozi na Wananchi  katika halmashauri zote na shughuli hii ya upandaji miti itaendelea kipindi chote cha mvua.

“Kila halmashauri inatakiwa kuweka msukumo wa kutosha wa kuwa na kitalu cha miche isiyopungua 1,500,000 ili kufikia lengo la kupanda na kuwa na ufanisi katika kutekeleza kampeni ya upandaji miti”. Madito

Akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe Reuben Mfune  amewataka viongozi wa serikali kushirikiana na wadau kusimamia ufuatiliaji utunzaji wa miti iliyopandwa kikamilifu pamoja na kupambana na wananchi wanaochoma moto hovyo misitu.

“Naamini kuwa ufuatiliaji imara utasaidia katika kuongeza uzalishaji na kuboresha ustawi wa miti iliyopandwa , aidha, nazitaka kamati za vijiji zinazosimamia mazingira kuongeza ufanisi katika kusimamia upandaji na utunzaji wa miti ili kuweza kupata manufaa”. Mhe Mfune

Naye Mwakilishi wa Meneja wa Misitu Kanda (TFS) Bibi Unice Mbilinyi amesema kuwa tayari wameanzisha bustani kila halmashauri kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali kulinda mazingira katika vyanzo vya maji.

Bibi Mbilinyi amesema TFS pia imepandaa miti kwa ajili ya kuwagawia wananchi na kusema kupanda miti huenda sawa na kutunza mazingira hivyo kuwataka wananchi kuhakikisha wanaitunza miti ambayo wanapanda kwenye mazingira yao.

Kampeni ya upandaji miti ni ya kitaifa ambapo hufanyika nchini kote kwa tarehe tofauti kulingana na misimu wa mvua katika kutekeleza Waraka wa Waziri Mkuu  kwa lengo la kupambana nakuenea kwa jangwa na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi, mkazo ukiwekwa katika kuhifadhi vyanzo vya maji na kuimarisha hifadhi ya mazingira.

Matangazo

  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza 2021 Mkoa wa Mbeya. December 18, 2020
  • Matokeo ya Kidato cha Sita 2020 August 21, 2020
  • Matokeo ya Darasa la Saba 2020 November 21, 2020
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • Watakiwa Kuongeza Kasi ya Ukusanyaji Mapato

    February 13, 2021
  • Halmashauri Zashauriwa Kujenga Shule za Waliofeli Kidato cha Nne

    February 11, 2021
  • Homa ya Mapafu Chanzo cha Kifo cha Dereva

    February 01, 2021
  • Mkoa wa Mbeya Wajiwekea Malengo ya Upandaji miti

    January 13, 2021
  • Tazama Zaidi

Video

Viongozi watakiwa kuwa wasafi
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Wasifu wa Mkoa wa Mbeya 2015
  • Mpango Mkakati wa Mkoa 2018-2023
  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Mpango Mkakati wa Kuendeleza Sekta za Kilimo 2020 - 2025
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Ajira

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Uzunguni Road

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025 2503034

    Simu ya Mkononi: 255 784838650

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2019 Mbeya Region . All rights reserved.