Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde: Juma Z. Homera amekagua Ujenzi wa Shule Tarajali ya Sekondari iliyoko Kata ya Kawetele Halimashauri ya Wilaya ya Rungwe na kuwataka Wananchi kuwa Wasimamizi na Walinzi wa Vifaa vya Ujenzi na Kwa wale wasio waaminifu kuacha mara Moja tabia ya Wizi kwa kuwa kufanya Kwao hivyo kutarudisha nyuma jitihada za Serikali.
Shule hiyo ambayo Wananchi wamechangia kwa Kununua eneo linalobeba Shule hiyo Kiasi Cha Sh. 7,900,000 na Kiasi Cha Sh. 2,500,000 kutumika kwenye Shughuli Mbalimbali imejengwa Mlimani ambapo RC Homera amesema itakuwa ni Moja ya Shule ya Mfano wilayani hapo na hii ni kutokana na Mazingira yake kuwa Mazuri.
Ujenzi wa Shule hii unagharimu Kiasi Cha Fedha Sh. 583,180,028 Fedha Kutoka Serikali kuu chini ya Mpango wa kuboresha Elimu ya Sekondari(SEQUIP) ambapo Mkuu wa Shule amesema Kukamilika kwake kutaondoa Changamoto ya Watoto Kusoma mbali na Makazi na hivyo kufanya Ufaulu wao kuimarika zaidi.
Ikumbukwe Kawetele ndio Kata Pekee katika Halmashauri ya wilaya ya Rungwe ambayo ilikuwa haina shule ya sekondari hali hiyo imewafanya wananchi kuipongeza Serikali kwa hatua madhubuti walizochukua za kuwajengea shule ambayo kwa hakika itakuwa fahari Kwa Kila atakayeiona.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa