Mkuu Wa Mkoa Wa Mbeya Comrade Juma Homera amekutana na Kuzungumza na Balozi wa India Nchini Tanzania Binaya Srikanta Pradhan Ofsini kwake Leo Desemba 09 2023.
Katika Mazungumzo Yao Wamejadili juu ya Uwekezaji katika sekta mbali mbali ikiwa pamoja na Kilimo (Balozi ameahidi kuleta wawekezaji kutoka India hivi Karibuni) na pia kujua maendeleo ya miradi ya maji inayotekelezwa katika mkoa wa mbeya chini ya ufadhili wa Exim Bank India na serikali ya India.
RC Homera pia amepata wasaa wa kuongea na Balozi kuhusu mafanikio ya ziara ya Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliye zuru India mwezi Oktoba mwaka huu.
Hata hivyo Homera amemwalika Balozi na Serikali nzima ya India kuendelea kuwekeza Tanzania(Mbeya) hasa katika nyanja za Kilimo, Uvuvi, Mifugo Biashara N.k.
Balozi ameahidi kumpa ushirikiano wa Kutosha RC Homera katika usimamizi wa miradi ya maji inayoendelea.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa