Waziri Wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh: Lela Muhamed Mussa na M/kit wa Kamati ya Bajeti Baraza la uwakilishi Zanzibar wamefika Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya na kupokelewa na Mkuu wa wilaya Mh:Beno Malisa kwaniaba ya RC Homera Lengo kuu ikiwa ni kusalimia na kueleza Dhima ya Ujio wao katika Mkoa huo.
Mh: Lela ameambatana na Wajumbe kutoka Chuo Cha State University of Zanzibar(SUZA) huku dhamila kuu ikiwa ni kutembelea Chuo cha sayansi na teknolojia Mbeya(MUST) na kujifunza juu ya Uendeshwaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi(HIT).
Mradi huo unaotekelezwa na Serikali kwa Ufadhili wa Bank kuu ya Dunia(WB) umelenga Kusomesha Wataalamu Kutoka vyuo mbali mbali nchini,
Kujenga majengo na
Kufanya maboresho ya Vyuo katika nyanja tofauti tofauti na Chuo cha MUST tayari washautekeleza Mradi huo kwa zaidi ya asilimia 75.
Akizungumza mara baada ya kuupokea ugeni huo Mh: DC Malisa amesema Mbeya Uongozi wa mkoa kupitia Chuo Cha MUST utaendelea kudumisha mahusiano bora na Chuo Cha SUZA hasa kubadirishana uzoefu katika Utendaji na uendeshaji ili kuinua Kiwango Cha taaluma Pande zote mbili(Tanzania bara na Zanzibar).
Hata hivyo ametoa wito kwa Wawekezaji Zanzibar kuja kuwekeza Mbeya kwakuwa ziko fursa Nyingi za kiuchumi(Biashara, Kilimo, Mifugo n.k) zinazoweza kuwafaa, zaidi kwenye Kilimo akagusia Ubora na upekee wa Mchele wa Mbeya.
"Mfano mchele wa Mbeya kama unavyofahamika ni mtamu sana, Nina Uhakika Chuo Cha MUST kishawapatia wakwenda nao hivyo tusaidieni kuwaeleza wawekezaji wa Zanzibar waje Mbeya kunufaika na haya Mambo mazuri mnayotasikia na mliyoyaona" Amesema Malisa
Mh: Lela ameshukuru kwa Mapokezi Mazuri aliyoyapata yeye na timu yake Kutoka kwa Serikali ya Mkoa wa Mbeya na Kwa uongozi wa Chuo cha MUST na kuahidi kuyachukua yale yote mazuri waliyoyapata chuoni na kuyafanyia kazi kadharika hakusita kuwaalika pia wenyeji wake kuitembelea Zanzibar kwaajiri ya kujifunza pia Mambo mbalimbali.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa