Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bwana Amour Hamad Amour amewataka Wananchi wa Rungwe kutumia fursa ya malighafi zinazopatikana Wilayani kuwekeza katika viwanda vidogo vidogo vya matunda kwa ajili ya kusindika na kuongeza thamani ya mazao yao ambapo vitaongeza pato kwa wananchi na Serikali.
Akiweka jiwe la msingi katika Kiwanda cha Matunda Ilenge Kata ya Kyimo Bw. Amor amesema kuwa kuwa Matunda yanayopatikana Rungwe kama hakuna viwanda wananchi hawataweza kunufaika na malighafi hiyo. Watanzania wana uwezo wa kuanzisha viwanda vya kuweza kusindika maparachichi, asali na kuondokana na dhana ya kulima malighafi hizo kwa wingi na kuziuza kwa bei ndogo na bidhaa zake kuuzwa ghali.
Aidha, kuanzisha viwanda vya alizeti kuuza yenyewe huwezi kupata faida, kuuza mafuta na chakula cha mifugo bei ya juu. kuangalia kuanzisha viwanda katika maeneo yetu. Wananwake wajitokeze
Afis Mtendaji wa Kata ya Kyimo Bw. Undule Mwasyonge amesema kuwa mradi wa Kiwanda cha Matunda utakapokamilika unatarajia kugharimu jumla ya sh. 1,058,665,900 ambapo kiasi cha Sh. 1,008,565,900 sawa na asilimia 95 za gharama za mradi ni fedha za ufadhili wa mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Sh. 5,000,000 ni fedha za Halmashauri.
Uledi amesema kwamba kukamilika kwa mradi huu kutasaidia kwa kiasi kikubwa wakulima wa matunda na mbogamboga kuhifadhi matunda yao kwa muda hata kuysafirisha nje ya nchiyakiwa yameongezewa thamani.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa