Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote wahakikishe kwamba maduka ya vyakula, dawa, vipodozi, machinjio zote, maduka ya nyama na samaki, migahawa na magari ya kubebea bidhaa hizi yakaguliwe mara kwa mara na hatua stahiki za kisheria zichukuliwe.
Mhe Makalla ameyasema hayo alipokuwa anafungua kikao cha Watendaji wa Mkoa na Halmashauri zote kuhusu uimarishaji wa utekelezaji wa majukumu ya TFDA yaliyokasimiwa kwa Halmashauri za Mkoa wa Mbeya kwenye Ukumbi wa Mkapa
Mhe Makalla Halmashauri zote hazifanyi kwa ufasaha kaguzi za mara kwa mara katika maduka mbalimbali ya bidhaa hizi, au vituo vya kutolea huduma, machinjio, maduka ya nyama na samaki na magari ya kubebea bidhaa hizi. Ninayo taarifa kuwa katika mkoa wetu ni machinjio MBILI ndizo zilizosajiliwa na TFDA.
Mhe. Makalla Tusitegemee mabadiliko kama tutaendelea kufanya kazi kwa mazoea. Ni budi tutambue kutambua lengo zuri la serikali la kupeleka madaraka zaidi ya utekelezaji wa majukumu ya TFDA kwa Halmashuri kuwa ni kuimarisha ufanisi wa udhibiti wa bidhaa husika. Ni vema kila mmoja akafanya sehemu yake kwa uweledi ili kuitendea haki taaluma yake na dhamana aliyopewa na jamii.
”Ninazo taarifa kwamba, makusanyo ya ada na tozo kwa huduma zilizokasimiwa, zitakusanywa ,zitabaki na kutumiwa 100% na Halmashauri.Hivyo ni kiasi cha kujua maoteo kiasi gani kinakusanya na kuingizwa katika mipango na bajeti za Halmashauri na mkoa pia ufuatilia mipango na bajeti za Halmashauri kama zinaonesha hili” . Mhe. Makalla
Mhe Makalla amesema kuwa wale wananchi au wafanyabiasha wanaofanya kwa makusudi biashara inayohatarisha afya za watanzania hata wale wanaosafirisha bidhaa zisizofaa kwa kificho katika magari ya mizigo au mabasi wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria na vyombo vya udhibiti na vya dola.
Mhe Mkuu wa Mkoa amesema Naamini TFDA na Halmashauri na vyombo vingine vya udhibiti mtashirikiana sana katika suala hili muhimu ikiwa pamoja na kutoa elimu zaidi kwa wananchi ili waweze kutambua kwa urahisi bidhaa zisizofaa na kwa wafanyabiashara ili waweze kutii sheria bila shuruti.
Meneja wa Mamlaka ya Chakula Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw Rodney Alananga amesema kuwa Halmashauri nyingi hazina takwimu kamili za majengo ya biashara za vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba. Halmashauri zetu pia zimekuwa zinasajili kwa kasi ndogo au hazisajili kabisa majengo yanayojihusisha na bidhaa zinazodhibitiwa na TFDA.
Bw. Alananga hadi sasa majengo ya chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba 1,511 ( 53%) kati ya 2851 yamesajiliwa na TFDA. Kati ya hayo yaliyosajiliwa, viwanda vya vyakula na vipodozi ni 55 ( vikubwa 19, vya kati 19 na vidogo17) .
Bw. Alananga Kazi kubwa bado ipo kwa viwanda vidogovidogo( micro) na vidogo(small) bado ambavyo vingi havijasajiliwa na tayari zipo juhudi kadhaa zimefanyika hasa kutoa elimu katika masuala mbalimbali ikiwemo ya usajili wa majengo na kanuni za usafi kwa mujibu wa sheria ya chakula, dawa na vipodozi Sura 219 uratibu ulioratibiwa na ofisi yangu ya Mkuu wa mkoa na taasisi mbalimbali za binafasi na serikali ikiwemo GS1, TFDA,TBS,SIDO,BRELA na wengine.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa