Kamishna wa Polisi Jamii CP FAUSTINE SHILOGILE leo Agosti 11, 2023 amekutana na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe.BENNO MALISA kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Comrade Juma Homera ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi katika mkoa wa Mbeya.
Kamishna SHILOGILE alipata nafasi ya kuongea na wajumbe wa kamati ya usalama ya Mkoa na Wilaya ya Mbeya kwa lengo la kuelezea falsafa ya Polisi Jamii, utekelezaji wa miradi ya Polisi Jamii hasa mradi wa Mkaguzi Kata na Polisi Kata.
Katika hatua nyingine Wajumbe wa kamati ya Mkoa wamemueleza Kamishina changamaoto wanazokutana nazo kwenye utendaji kazi katika jamii ambapo mojawapo ni Ndoa za Utotoni zinazochangiwa na Viongozi wa Dini wasio na vigezo kuzifungisha ndoa hizo makanisani mwao.
Kigongo Shile ni Kamishina Msaidizi wa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya(RIO) amesema moja ya changamoto alizoshuhudia ni ya Wananchi kujichukulia hatua ya kumpiga Mtu na kuondoa maisha yake pasipo kujiridhisha kama ni mkosaji hivyo ameliomba Jeshi la Polisi kuwa makini na shapu hasa wasikiapo matukio kama hayo.
Beno Malisa amemshukuru Kamishina Shilogile kwa kuona vema kufika katika ofisi za Mkoa wa Mbeya na kukutana na kuwasikiliza wajumbe wa Kamati ya Usalama baadhi ya Changamoto zinazowakabili.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa