Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. John Jingu amefanya ziara Mkoani Mbeya na kukagua maendeleo ya zoezi la anwani za makazi ambayo bado yanaendele kufanyika na kulipongeza jiji la Mbeya kwa hatua kubwa waliyoweza kuifikia.
Dkt. Jingu ameyasema hayo wakati akikagua karakana ya kutengeneza nguzo na vibao vya anwani za makazi katika eneo la soweto jijini Mbeya alipoambatana na kamati ya utekelezaji wa zoezi hilo.
Aliweza pia kutembelea wilaya ya Rungwe na Kyela ambapo zoezi hilo linaendelea kufanyika na kuridhishwa na hatua waliyoweza kufikia ambapo vibao vya mitaa na namba zinaendelea kuwekwa.
Uzunguni Road
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025 2503034
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Copyright ©2019 Mbeya Region . All rights reserved.