Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amewataka wamiliki wa kiwanda cha East African Starch Ltd kuongeza kasi ya ujenzi mpaka Desemba 2018 kama mipango kazi unavyoonyesha
Mhe. Makalla ameyasema hayo alipotembelea kiwanda hicho na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ili kukagua maendeleo ya kiwanda hicho ambacho kabla ya kubinafsishwa kilikuwa kinaitwa Mbeya Textile.
Mhe. Makalla amesema kuwa uwekezaji wa kiwanda hiki unathamani ya shilingi bilioni 50 na kitazalisha bidhaa za viwandani ktk viwanda vya vyakula, vinywaji ,chocolate pia kitazalisha mafuta na vyakula vya mifugo.
Amesema kuwa Kiwanda hiki kitakuwa kikubwa na pekee Afrika mashabiki na kitasaidia kupata kana kwa soko la mahindi kwa wakulima wa nyand a za juu kusini.
Mhe Makalla amesema kuwa Kiwanda hiki ni uboreshaji wa kiwanda cha Zamani cha Mbeya Textile ambacho kilisimama baada ya kukosa malighafi ya Pamba.
Amesema kuwa Seikali ilipiga marufuku kilimo cha pamba Mkoa wa Mbeya tangu mwaka 1994 baada ya kuwepo kwa funza mwekundu ambaye aliathiri kwa kiasi mkubwa kilimo cha pamba.
Kutokana na kukosekana na kwa malighafi ya pamba Wizara ya Fedha kupitia Msajili wa Hazina walimruhusu mwekezaji kubadilili matumizi na sasa kiwanda kitatumia malighafi ya mahindi
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa