Uharibifu wa mazingira kwa ukataji wa miti hovyo na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu pembezoni mwa mto Mbarali zimekuwa sababu kubwa zinazochangia kupunguza kiasi cha maji kuelekea mto Ruaha na pia kubadilisha muelekeo wa maji ya mto huo.
Hayo yamebainishwa na Kikosi Kazi cha Kitaifa kunusuru Mto Ruaha wakati wakisikiliza maoni na changamoto kutoka kwa wadu mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.
Akiongea na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha kunusuru Mto Ruaha ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Richard Muyungi amesema kuwa kuna uvamizi mkubwa wa wakulima katika mfereji wa kampuni ya Mbarali Estate ambao unaotoa maji kwenye mto kupeleka katika mashamba yao ambapo unasababisha utumiaji wa maji holela wa maji katika wilaya ya Mbarali.
" Mfereji unaotoa maji kutoka Mto Mbarali kuja kwenye mashamba umejengwa kwa umbali wa Km.14 ambapo hapo katikati wananchi wanatumia pumpu kuchukua maji kwa ajili ya kumwagilia mashamba yao ambayo ni makubwa sana".
Aidha, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi Mariam Mtunguja ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kuhakikisha wana kamata mashine zote za kusukumia maji kutoka mfereji wa shamba la mwekezaji mpaka kwenye mto. Mifereji na mabanio yanachepusha maji bila kibali katika Wilaya ya Mbarali yapelekea kukatika kwa Mto wa Ruaha.
Bibi Mtunguja amewataka Watendaji wa Vijiji na Kata kutoa Elimu kwa Wananchi wa Maeneo yao juu ya matumizia sahihi ya maji na juu ya sheria ya kufanya shughuli za kibinadamu mita 60 toka kingo za mto ili wapate uelewa zaidi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Bw. aamesema kuwa uanzisahaji wa Mashamba makubwa yanayochepusha maji kutoka Mto Mbarali na kupeleka kwenye mashamba hayo kunasababisha upotevu wa muelekeo wa maji ya Mto Mbarali unaopeleka maji yake Mto Mkuu Ruaha na kusababisha uchache wa maji yanayoelekea mtoni.Mto.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa