Wananchi wa Jimbo la Lupa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Wametoa Hisia zao Njema kwa Serikali baada ya Gharama za Upatikanaji wa Maji kupungua Kutoka Shilingi 500 mpaka Shilingi 25 kwa NDOO Moja.
Wananchi wameyasema hayo Mbele ya Mwenge Wa Uhuru ukiongozwa na Kiongozi wa Mbio hizo Ndg: Godfrey Mnzava Pamoja na Jopo lake wakati akiweka Jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Maji unaotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)
Godfrey Mnzava amewaomba Wananchi kulinda na kutunza Miundombinu hiyo ya Maji wakati huo Serikali ikiendelea kumalizia Ujenzi wa Visima Vingine vinne vilivyobaki kupitia kwa Wakala wake!
RUWASA imetekeleza Ujenzi wa Mradi huo ikiwa ni Program Maalum ya Nchi Nzima ya kujenga Visima vya Maji ambapo kwa Jimbo la Lupa kisima kimoja Kati ya Vitano tayari kimejengwa kwa Gharama ya Milioni 123.
Aidha RUWASA inapaswa Kuchimba Visima Vitano katika Jimbo hilo la Lupa ambavyo Gharama zake ni Milioni 499.
Mchanganuo wa Gharama za Ujenzi wa Kisima hiki ni Pamoja na:
Kununua Pampu
Kununua Solar
Kununua Mabomba
Kujenga Point Source.
Mbunge wa Chunya Mh:Masache Njeru Kasaka Ameoupongeza Mwenge wa Uhuru Kwa kuendelea Kutoa Nuru kwa Wananchi wa Jimbo la Lupa sawa sawa na Dhamila Njema ya Mh: Rais Dr. Samia Suluhu Hassan
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa