Kampuni ya GSM kupitia kampuni tanzu ya GS Agro imemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila mifuko 140 ya mbolea kwa ajili ya vikundi 7 vya wanawake kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Akimpokea mbolea hizo leo ofisini kwake Mhe. Chalamila ameishukuru kampuni hiyo na kuwaomba kuendelea kusaidia kwa kadri itakavyoendelea kuguswa katika kusogeza mbele maendeleo ya kiuchumi kwa upana wake.
Mhe. Chalamila amesema vikundi saba vitakavyonufaika ni Palishimo, Uhalamsye, Mwawesya, Zinduka, Lwangaje, Wile na Tashila na ambavyo vitapokea mifuko 10 kwa kila kikundi
Chalamila amesema mkoa umeshaanza mazungumzo na nchi jirani za Congo na Zambia kwa ajili kutafuta masoko ya mazao na hivyo kuwataka wakulima hao kutumia mbolea waliopewa msaada.
Mhe. Chalamila amesema amewaomba GSM waje kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya magodoro na misumari vitakavyoweza kuongeza ajira na mapato kwa Mkoa wa Mbeya.
Bibi Marieta Ben Mwakilishi wa kina mama ameishukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuweza kiwaombea mpaka kampuni ikakubali kuwasidia kupata mbolea hiyo na kusema itawapunguzi tatizo la kuwa magolikipa katika ndoa zao kwa sababu sasa wana uwezo wa kujitegemea.
Akikabidhi mbolea hizo Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni ya GSM Bw. Martina Nkuru ametoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa na kusema kuwa hizo ni jitihada zake alizozifanya kwa ajili ya wananchi wake na kampuni mpaka ikaona umuhimu wa kusaidia katika harakati zake za kuinua uchumi wa Mbeya.
Bw. Nkuru amesema kuwa kampuni imeanza kwa kuwasidia wakina mama wa vikundi vinavyojishughulisha na kilimo kama mwanzo wa kuanza kujenga mahusiano mazuri na Serikali na kuomba makampuni mengine kuendelea kuiga mfano wao.
Nkuru amesema kuwa kampuni itaendelea kutoa misaada mingine hasa katika masuala ya uwekezaji wa viwanda.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa