Mkandarasi wa Kampuni ya M/S CHAGATU EARTH WORKS CO LTD, ameaswa kumaliza kwa Wakati Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Masundo katika Barabara ya Kambasegela-Nsundo-Ntaba yenye urefu wa Km. 6.31 iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.
Rai hiyo imetolewa na Mwenge wa Uhuru 2024 kupitia kwa Kiongozi wake Ndg: Godfrey Eliakim Mnzava wakati Mwenge wa Uhuru ulipokagua na kuweka Jiwe la Msingi Mradi huo na kumuasa Mkandarasi kuwa hakuna muda utakaoongezwa Nje na Makubaliano ya kwenye Mkataba.
Ujenzi wa Daraja Ulianza mara baada ya kukosekana kwa Mawasiliano ya Muda mrefu ya Barabara ya Kambasegela-Masundo na Ntaba na Ulianza Kutekelezwa Tarehe 19/05/2023 na ulitarajiwa Kukamilika Tarehe 18/05/2024 muda wa Miezi Nane(8).
Mradi huu unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania kupitia Fedha za Tozo ya Mafuta kwa Gharama ya Shilingi 458,358,707.50 ulitengewa Bajeti ya kiasi Cha Shilingi 500,000,000 na tayari Maombi ya Malipo ya awali kwa Mkandarasi yameshatumwa ambayo ni kiasi Cha Shilingi 351,228,901.25.
Mradi huu utakapokamilika Utahudumia wananchi wapatao 14,166 kwa Kata za Kambasegela na Ntaba na itawarahisishia Wananchi kusafiri na kusafirisha Mazao Yao Kutoka Mashambani kupeleka sokoni na Maeneo mengine ya Kibiashara.
Kauli mbiu ya Mwenge Wa Uhuru 2024 ni Tunza Mazingira Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa endelevu.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa