• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Halmashauri ya Mbeya yapongezwa Kwenye Ukusanyaji Mapato

Imetumwa : June 26th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kushika nafasi ya kwanza kati ya halmashauri Saba za Mkoa katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ambapo hadi Mei 31, 2019 kiasi cha sh. 3, 516,444,947.00 sawa na asilimia 118.87.                                                                   Mhe Chalamila ameyasema hayo leo kwenye kikao cha Baraza maalumu la Kupitia hoja za Mkaguzi Mkuu wa Serikali na kuwataka kuendelea jitihada za kukusanya ili ifikapo Juni 30, 2019 halmashauri ifikie asilimia kubwa zaidi na kuendelea   kuongoza.                                                                “Hata hivyo kutokana na ukomo wa bajeti yenu, ni vema mkaandaa maelezo ya kutosha kuhusu makusanyo ya mapato ya ndani yanavyoongezeka zaidi ya mlichopanga kukusanya ili kuweka kumbukumbu zenu vizuri na kuweka uelewa wa kutosha kwa watumiaji hesabu zenu pia kumtosheleza mkaguzi anapopita kuwakagua”. RC Chalamila.                     Mhe Mkuu wa Mkoa ameendelea kusema jukumu la ukusanyaji mapato ni la watendaji na Madiwani, hivyo hakuna budi kutumia uwezo wenu kuhakikisha kwamba mapato yanapanda na kishirikiana na wadau wengine katika kutafiti na kubuni vyanzo vipya vya mapato.                                                         Aidha, Mhe Chalamila amesema kuwa kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ni lazima kuendane na nidhamu ya matumizi hivyo ni jukumu la Madiwani kuhakikisha kuwa mapato yote yanakusanywa kutoka kwenye vyanzo vya ndani na ruzuku ya Serikali yanatumika katika malengo yaliyokusudiwa.                                Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bw Paul Ntinikaamesema kuwa anajivunia kuwa na halmashauri ambayo inashika nafasi ya kwanza kwa ukusanyaji wa mapato  na kusimamia ipasavyo matumizi ya mapato hiyo na kufanya halmashauri hiyo kupata hati safi.                                                 Bw. Ntinika amesema kuwa halmashauri ya Mbeya pia imeweza kutoa zaidi ya milioni 400 za asilimia 10 kwa ajili ya kinamama, vijana na walemavu na kufanya halmashauri hiyo kutoa fedha zote za za 10% katika bajeti ya mwaka 2018/2019.                                                       Naye Mwenyekiti wa halmashauri Mhe Mwalingo Kisemba amemshukuru Mkuu wa Mkoa na kusema kuwa hiyo inatokana na ushirikiano mzuri kati ya watumishi wa halmashauri na Baraza la Madiwani na kuahidi kuongeza kasi hiyo ya kukusanya mapato na kubuni vyanzo vipya.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA IMES

    April 29, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YARIDHISHWA NA MAJIBU YA WADAU KUHUSU MAPENDEKEZO UGAWAJI WA JIMBO LA MBEYA MJINI.

    April 25, 2025
  • DKT. HOMERA AAGIZA MRADI KUKAMILIKA HARAKA IWEZEKANAVYO ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA

    April 14, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa