Mkuu wa wilaya ya Mbarali kanali Maulid Surumbu aitakaka jamii kuwalinda na kuwajali wazee kwakuwa wazee ni tunu ya katika jamii yeyote ile
Rai hiyo imetolewa wakati wa hafla ya siku ya wazee kimkoa iliyofanyika katika mkoa wa Mbeya ambapo Kanali Maulid Surumbu amihamasisha jamii kuwa na upendo kwa wazee
Aidha Mwenyekiti wa Baraza la ushauri la wazee mkoa wa Mbeya Urther Mwankenja kwaniaba ya baraza la ushauri mkoa wa Mbeya wameishauri serikali mambo mbalimbali ya kuyafanyia kazi kwa wazee ikiwemo kuboresha malipo ya pensheni kwa watumishi ambao walisha staafu ili waweze kujikwamua kiuchumi
Kwaupande wake Mwakilishi kutoka Hospitali ya Rufaa kanda Mbeya Digna Kikasi amesema Hospitali hiyo imeboresha kwakiwango cha juu utoaji wa huduma kwa wazee huku akibainisha baadhi ya huduma zinazotolewa kwa wazee katika Hospitali hiyo
Pia Mwakilishi kutoka ofisi ya Bima (NHIF ) Nikolaus Mwangomo ametoa Elimu ya umuhimu wa Bima ya Afya kwa wazee
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa