Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt Yahya Msuya amewataka waandishi wa habari kuwa daraja la kufikisha wananchi elimu juu ya mapambano dhidi ya Kipindupindu katika Halmashauri za Mkoa wa Mbeya.
Akiongea katika semina ya kudhibiti kipindupindu ya waandishi wa habari wa radio Dkt. Msuya amesema kuwa Mkoa umeendelea kukabiliana na Kipindupindu katika Halmashauri za Mbarali na Chunya.
Dkt. Msuya amesema kuwa katika kufikia mafanikio yaliyopatikana katika kudhibiti ugonjwa huu Mkoa umetumia mbinu mbalimbali ikiwa pamoja na kuimarisha eneo la tiba pamoja na kinga.
" Eneo la tiba limehusisha kuandaa maeneo ya kupokelea wagonjwa na kuwa na watumishi wa kutosha katika maeneo hayo, kutoa huduma stakihi, kuwa na dawa za kutosha." Dkt. Msuya
Dkt. Msuya amesema kuwa Mkoa umepanga kuimarisha Mkakati Kipindupindu kwa kushirikisha vyombo vya Habari na Viongozi wa Serikali na Siasa ili kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ya jinsi ya kupambana na Kipindupindu.
Akichangia katika semina hiyo Mwandishi Yosia Sinkala ameshauri Mkoa kuandaa mikutano ya hadhara kuanzia ngazi ya vijiji Mitaa na Kata kwa ajili ya kutoa elimu jinsi ya kupambana na ugonjwa wa Kipindupindu.
Bw. Sinkala amesema kuwa viongozi wa Vijiji na Kata wana ushawishi kwa wananchi wao hivyo ni muhimu kuwashirikisha kutoa elimu hiyo kwa wananchi ya mapambano dhidi ya Kipindupindu na pia kutarahisisha utoaji wa taarifa ya wagonjwa.
Naye Bw. Ezekiel Kamanga wa Ebony Fm ameshauri kuwa waandishi waandae vipindi mbalimbali katika redio kuhusu jinsi ya kupambana na Kipindupindu na kuandaa makala mbalimbali za redio kuhusu uginjwa huo.
Bw. Kamanga amesema kuwa waandishi watatembelea maeneo mbalimbali yaliyoathirika na ugonjwa wa kipindupindu na kuandaa makala ambazo watazirusha katika redio na kuwawezesha wananchi kuanza kujilinda na ugonjwa huo.
Aidha, Samuel Mhando wa Dream Fm kashauri kuandaa dawati katika ngazi ya Kata na Vijiji yatakayohusisha wananchi na Wataalamu wa Afya ambao watakuwa wanasimamia utoaji wa elimu kuhusu Kipindupindu katika maeneo Yao.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa