Serikali kupitia mradi wa umeme wa REA Awamu ya tatu imepanga kupeleka huduma za umeme katika Kata mbili za Nkokwa na Ipande wilayani Kyela ambazo hazikufikiwa na mradi huo kuanzia mwezi aprili mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati Mhe. Dr. Medard Kalemani katika ziara yake ya kikazi wilayani humo kwa lengo la kukagua shughuli za masuala ya nishani.
Dr Kalemani amesema kuwa Serikali imedhamiria kwa nia ya dhati kumaliza taizo la umeme katika Wilaya hiyo kwa kuhakikisha kata zote 33 zinapata umeme pamoja na vijiji vyake vote.
Amesema kuwa Wizara imejipanga kupeleka umeme katika taasisi zote za Serikali na zisizo za kiserikali zikiwemo shule, Zahanati,makanisa,misikiti na mitambo mbalimbali inayohitaji nishati.
Hata hivyo Mhe, Waziri hakusita kuzungumzia matatizo wanayoyapata Wananchi wa Mkoa wa Mbeya, mfano kukatika kwa Umeme Mara kwa Mara, watu kuchelewa kuunganishwa na huduma ya umeme hata kama wamelipia.
Dr Kalemani amesema kuwa Serikali inaamini hadi kufikia mwaka 2021 Tanzania yote itakuwa na umeme na kupeleka urahisi wa shughuli za maendeleo ya nchi ili kuipeleka nchi yetu katika uchumi wa kati.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa