Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2018 Ndugu Charles Kabeho ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya kuweza kuwahudumia wananchi8 hasa kwenye sekta ya maji ikiwa ni sera ya wizara ya kuwa na maji ndani ya mita nne.
Bw. Kabeho ametoa pongezi hizo wakati akizindua mradi huo wa maji na kuwapongeza wananchi pia kwa kuchangia ujenzi wa mradi ambao utawahudumia wananchi 1,436 wa kijiji hicho ili kondokana na tatizo la maji lililiokuwepo.
Bw Kabeho amesema kuwa Serikali ya Awamu ya tano imedhamiria kumtua mama ndoo kichwani kwa kusogeza miradi ya maji karibu na vijiji na kuondoa kabisa tatizo la kufuata maji umbali mrefu.
Aidha, Bw. Kabeho ameitaka halmashauri hiyo kusimamia miradi ya maji kwa ukaribu ili kuwezesha ujenzi wa miradi hiyo kuendana na thamani ya fedha za wananchi na Serikali zinzotolewa.
Akisoma taarifa ya mradi Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilamba amesema kuwa mradi wa maji Ilamba ulipangwa kutekelezwa kwa gharama ya shilingi 178,000,000 kwa ufadhili wa Serikali kuu na mchango wa nguvu za wananchi kiasi cha shilingi n1,900,000.
Mhe Mwenyekiti amesema kuwa hadi mradi unakamilika umegharimu jumla ya shilingi 134,072,685.84 ikiwemo mchango wa nguvu za wananchi shilingi 1,900,000 kwa ujenzi wa chanzo cha maji, tenki la kuhifadhia maji, vituo 13 vya kuchotea maji na kuchimba mitaro.ugo kuwa katika hatari ya kuliwa na mamba.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa