Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Bwn, Yusuph Juma Mwenda Leo October 08,2024 amekutana na Kufanya Mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde: Juma Z. Homera Ofsini kwake Namna ya Ukusanyaji Mapato Kwa Mkoa huo pasipo bugudha.
Kamishina amesema wao wanaendelea kufanya maboresho katika ukusanyaji Kodi kwa Wafanyabiashara "Na Sitarajii kuona Zoezi hili linakuwa chanzo au Kichocheo Cha ugomvi na utata Kati ya Mlipaji na Mkusanyaji bali tutajikita zaidi katika Utoaji Elimu kwa Walipaji kabla ya kuwatoza" Amesema Mwenda mara baada ya Kusaini Kitabu Cha Wageni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa..
Aidha amesema Ujio wake mbali na kujitambulisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa lakini pia umeambatana na Ziara ya kutembelea na Kuzungumza na Wafanyabiashara Mbeya na Madereva Walioko Mpakani Kasumulu.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde: Juma Z. Homera amesema Mkoa wa Mbeya uko salama Mahusiano kati ya Wafanyabiashara na Serikali Yako Vizuri kafharika Mbeya na Nchi Jirani hakuna utata wowote.
Homera amesisitiza kuhusu Bandari kavu ya Mbeya Malawi Cargo Kuanza kufanya Kazi ili kuifanya Mbeya kuimarika zaidi kiuchumi na Kongeza Mapato kupitia Uagizaji wa Mizigo Kutoka kwa Wafanyabiashara kupitia Bandari hiyo na ikiwezekana Siku za Mbeleni Ijengwe Reli ya kuunganisha Nchi hizi mbili.
Ikumbukwe Wiki kadhaa Nyuma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt: Samia Suluhu Hassan kupitia Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde: Juma Z. Homera alitangaza msamaha wa kutolipa Faini kwa MADEREVA MALORI waliokuwa wakisafirisha Vyumba chakavu kinyume na Utaratibu vikitokea Malawi Kuelekea nchini Congo kupitia Mpaka wa Kasumulu.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa