Ngozi ni ziwa la kreta (crater lake) lipatikanalo Mkoa wa Mbeya kwenye milima ya Uporoto, lipo katika nyuzi 9.008° Kusini na 33.553° Mashariki, ni ziwa la pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya lile lililoko nchini Ethiopia. Hata hivyo, wataalamu wanasema kwamba Ziwa Ngosi lina sifa za kipekee linazolitofautisha na lile lililoko Ethiopia.
Moja ya tofauti hizo ni kwamba Ziwa Ngozi lina umbo ya ramani ya Afrika na limezungukwa na milima na misitu minene tofauti na lile la Ethiopia ambalo liko eneo lililo wazi na hufikika kwa urahisi kabisa kwa gari kitu ambacho hakiwezekani kwa Ziwa Ngosi.
Wataalamu wanasema kwamba kuwepo kwa ziwa hilo sehemu hiyo kunasaidia kuzuia milipuko ya mara kwa mara ya volkano kwa kuwa linasaidia kupunguza misukumo ya gesi inayojijenga chini na kuanza kutafuta upenyo wa kutokea chini ya ziwa.
Ziwa hili pia lina ingiza tu maji na halitoi maji kwa sababu liko katikati ya milima hivyo kuonekana kama liko shimoni alafu halina ufukwe, ziwa hili linalopatikana katika Hifadhi ya msitu Uporoto (Poroto Ridge) yenye eneo la hekta 9,332 ipatikanayo karibu na vijiji vya Kisanga 4.3km Uyole (24.4km) na mji mdogo wa Tukuyu upatikanayo wilaya ya Rugwe.
Zipo imani nyingi potofu juu ya ziwa hilo la maajabu watu husema ziwa hili lilichomwa moto na wakazi wa kijiji cha Mwakaleli kwasababu lilikuwa likileta mikosi mingi kijijini hapo ikiwemo vifo vya mara kwa mara kitu ambacho si sahihi kitaalam ziwa haliwezi kuhama,
Zipo imani miongoni mwa watu kuwa ziwa ngosi watu wanapotea kimazingara, kuwapo kwa sauti za watu wasioonekana ndani ya misitu, wengine husema ziwa hilo limekuwa likigeuka rangi mara kwa mara na kuwa na rangi za kijani, bluu, nyeusi na nyeupe.
Chanzo: Mbeya Tourism Blog
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa