Katibu Tawala Msaidizi Idara ya Mipango na Uratibu Noah Sikwese amewaelekeza Maafisa Maendeleo ya Jamii kuhakikisha wanajifunza na kuufahamu Mfumo wa IMES utakaotumika kwaajiri ya uwasilishaji wa Taarifa za Sekta ya Maendeleo ya Jamii.
Sikwese amewaambia Maafisa hao kuwa mara baada ya Mafunzo nao watatakiwa kwenda Kutoa Elimu kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Halmashauri na Kata hivyo ni Vema wakatilia mkazo katika kujifunza ili watoapo Elimu ikawe ya Ukweli na Uhakika na yenye kuleta Mafanikio katika Jamii.
Ameyasema hayo Leo April 29,2025 wakati akifungua Kikao Kazi Cha Maafisa Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Aidha amewataka washiriki wa Kikao kuhakikisha wanainviza takwimu Sahihi kwenye Mfumo kwakuwa ndizo zinazousaidia Mkoa na Halmashauri kupanga Mipango na bajeti.
Kabla ya kuhitimisha Hotuba yake Sikwese akawataka washiriki kutekeleza Majukumu Yao kwa Mujibu wa Mwongozo wa Utekelezaji wa Majukumu ya Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa