Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Kyela kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuboresha vyanzo vilivyopo ili kuwezesha Halmashauri kuweza kuongeza uwezo wa kujitegemea kwa mapato ya ndani ya halmashauri
Mhe. Amos Makalla ameyasema leo alipofanya kikao maalumu cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri YA Kyela kujadili ripoti ya CAG mwaka wa fedha 2015/16
Mhe. Makalla amewataka pia Waheshimiwa Madiwani kutenga maeneo YA uwekezaji kwa ajili YA viwanda vidogo, kati na vikubwa kufanya hivyo kutaongeza Mapato YA halmashauri na serikali kuu
Amewaeleza madiwani kuhamasisha wakulima kuongeza uzalishali wa mpunga na wajasiriamali kuongeza thamani mchele na mchele wa kyela katika vifungaishio vizuri kufanya hivyo kutaongeza soko na kkuongeza mapato kwa Halmashauri.
Aidha, Mkuu wa Mkoa amewataka Madiwani kuendelea kuwaunganisha wakulima kwenye vyama cha ushirika ili wakulima waweze kunufaika na kilimo cha na Halmashauri iweze kuongeza mapato.
Amesema halmashauri ikiboresha mapato itasaidia halmashauri kutoa huduma za jamii kwa wananchi ikiwemo afya, elimu, Maji nk na pia kiwango cha mikopo kwa vikundi vya vijana na wanawake itaongezeka
Mhe. Makalla amesema kuwa ukusanyaji wa mapato ya ndani lazima uendane na nidhamu ya matumizi ya fedha kwa hiyo ni jukumu la Baraza la Madiwani kusimamia na kuhakikisha kuwa mapato yote yanayokusanywa katika vyanzo vya ndani yanatumika ipasavyo.
Ufuatiliaji wa mara kwa mara ufanyike ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa na lazima Waheshimiwa Madiwani utaratibu wa kukagua miradi hiyo inayotekelezwa na Halmashauri kupitia kamati zako.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa