Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amezita kamati za ulinzi na usalama ngazi zote na wananchi kulinda hifadhi za msitu ya asili kwani ni vyanzo vikubwa vya maji na uoto wa asili.
Mhe Makalla ameyasema hayo leo wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa kukagua hali ya misitu ya hifadhi yalima Rungwe, Uporoto na Sawago
Mhe. Makalla amesema kuwa ni marufuku shughuli zote za kijamii ktk misitu yote ya hifadhi ikiwemo uwindaji, kilimo, ukataji miti na uchomaji moto misitu.
Aidha Mwenyekiti wa kamati hiyo ameielekeza TARURA halmashauri za Rungwe na Mbeya kuboresha miundombinu kwa ajili ya kuwezesha watalii kufika kwa urahisi ktk ziwa Ngozi, Daraja la Mungu na hifadhi za Mlima Rungwe.
Naye Mwenyekiti wa Kitongoji cha Honde Bw. Waziri Benard amesema kuwa viongozi wa kijiji na Kata wameendelea kusimamia utunzaji wa msitu huo ijapo kunakuwa na changamoto za watu wachache kuendelea kuharibu.
Bw. Benard ameiomba Serikali kuweka alama za mipaka kwenye eneo la hifadhi ili kurahisisha usimamiaji wa eneo hilo.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa