Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amewataka wananchi wa Kata ya Iyela kuacha Siasa ili waweze kupeleka maendeleo ya ujenzi wa madarasa katika Kata zao.
Mhe. Makalla ameyasema hayo alipokuwa akikabidhi mifuko 100 ya sementi shule ya msingi Iyela kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.
Mhe Makalla amewataka wazazi kuwa na ushirikiano na Serikali ili kuweza kumaliza tatizo la upungufu wa madarasa katika shule za Msingi na Sekondari Mkoani Mbeya.
Amesema kuwa viongozi wa Kata kuacha urasimu wa matumizi ya mifuko ya simenti na kuhakikisha inatumiwa ipasavyo kwa matumizi yalioainishwa.
Mdau wa Elimu Mkoa wa Mbeya Be. Ndele Mwaselela ameahidi kutoa mabati kwa ajili ya madarasa mawili na matofali 1000 kwa ajili ya kuendekeza ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Iyela.
Bw. Mwaselela amewaomba wananchi kuendelea kuchangia mchango wa ujenzi wa shule na kuahidi kuendesha zoezi la uchangishaji katika kata hiyo.
Aidha, Bw. Mwaselela amemahidi Mhe. Makalla ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wadau wa elimu Mkoa wa Mbeya pale changamoto za masuala ya elimu yatakapojitokeza.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa