Mwenge wa Uhuru 2024 kupitia kwa Kiongozi wake Ndg: Godfrey Mnzava umewaagiza Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala (W) Kusimamia kwa Ukaribu na umakini Mfumo wa manunuzi unaotumika katika Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwenye Maeneo Yao.
Mnzava Amesema adhamila ya Mh: Rais na Serikali Nzima ni kuona uthibiti wa Upotevu wa Mapato hasa katika Ununuzi hivyo ni Vema wakalisimamia Agizo la Mh: Rais la kuhakikisha hakuna ubabaishaji utakaojitokeza katika Utekelezaji wa Miradi hiyo.
Hayo ameyasema wakati Leo wakati akiweka Jiwe la Msingi katika Daraja la Imezu lenye urefu wa Mita 7 upana wa Mita 5.7 na kina Cha Mita 4 katika Barabara ya Imezu-Darajan Kata ya Inyala.
Ujenzi wa Daraja hilo umegharamiwa na Fedha za matengenezo ya Barabara kiasi Cha Sh. 118,531,440.00 na Fedha iliyolipwa kwa Mkandarasi 82,420,040 sawa na 69.5% ya Mkataba wake.
Kumalizika kwa Daraja hili la Imezu kutarahisisha Usafiri na usafirishaji wa haraka wa Mazao kutoka Kata ya Inyala na Nje ya Kata hiyo kwenda Sokoni kadhalika Daraja hili litachochea Shughuli za kiuchumi ajira na Kipato kwa Wananchi wa Kata za Inyala na Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Utekelezaji wa Mradi huu hadi Sasa umekamilika kwa asilimia 80.69%.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa